MACHAPISHO MBALIMBALI YA MAMA ELLEN G. WHITE
TOKENI MIJINI
E. G. White
Msaada kwa Maadili na Usalama wa
Jamii
Mkusanyo wa Maandiko
ya
ELLEN G. WHITE
Mfasiri: M. Mwamalumbili
Country Living - Kiswahili
DIBAJI
Faidaza kuishi shamba [vijijini] zimesisitizwa tena na tena katika mashauri yanayotolewa na Roho
ya Unabii. Mawingu ya dhoruba yanayojikusanya yanaashiria kwamba yafaa kuanza kupaza sauti
ili kutoa wito wa kuihama miji. Ni budi iwe wazi kwa kila Mwadventista Msabato mweny e akili
kujua ya kwamba kuishi mjini, pamoja na msongamano wa watu uliopo, vishawishi vyake na
migogoro ya vyama vya wafanyakazi inayozidi kuongezeka, hakuweki mazingira yenye kuleta afya
kwa familia za Kikristo.
Kwamiaka mingi maelfu ya Waadventista Wasabato wameelekezwa kuchagua mazingira
yanayofaa kuweka makazi yao na katika uhusiano wao na mashirika ya ulimwengu kwa njia ya
mashauri yatokanayo na shuhuda juu ya mambo hayo ya maana sana ambayo yamechapishwa na
kutawanywa katika sehemu nyingi. Ishara m baya za hatari kubwa iliyo karibu sana kutokea
zinapoonyesha ugumu wa kuzitambua hatari hizo na ukali mno wa pambano lililo mbele yetu,
inaonekana kwetu ya kwamba ni jambo linalofaa kuuchapisha tena ushauri huu kwa kutumia
mtindo huu ambao unaweza kuyanasamawazo ya kila mshiriki wa kanisa.
Nakwa kufikiria nyakati hizi tulizo nazo [hivi sasa], ni mahali pake, sio tu kurudia ushauri ule
unaofahamika sana uliochapishwa muda mrefu uliopita, bali kuzitilia nguvu semi hizo kwa kuzitoa
kwa mafundisho ya kinagaubaga yaliyopata kuchapishwa toka wakati hata wakati katika gazeti la
Review and Herald au yaliyoandikwa katika barua zake za ushauri zilizoandikwa kwa watenda kazi
waliokabidhiwa madaraka katika kazi ya Mungu. Kitendo kama hicho kinapatana kabisa na
maagizo ya Bibi E. G. White kwa wadhamini wake ili waweze kutayarisha "kwa ajili ya
kuchapishwa maandiko yangu yaliyokusanywa pamoja kutoka katika maandiko yangu ya mkono,"
kwa maana, kama alivyosema yeye mwenyewe yana "maagizo aliyonipa Bwana kwa ajili ya watu
wake." Mwaka wa kuandikwa au kuchapishwa kwa mara ya kwanza umetolewa pamoja na
kumbukumbu ya chanzo cha kila kifungu cha maneno [kilichotumika].
Witowa dhati uliotolewa katika kijitabu hiki unataka pawepo na nia ya kutekeleza jambo hili,
lakini [kwa wakati uo huo] onyo hili zito linatolewa ili watu wetu wasithubutu kukurupuka
[kufanya mambo bila kufikiri na kupanga vizuri]. Tungependa kuyaelekeza mawazo yenu hasa kwa
tahadhari zile zinazopatikana katika Sehemu ya Saba, "Kuongozwa kwa Maongozi ya Mungu, "
ambayo inatokea kwenye kurasa za . Kijitabu hiki sasa kinawekwa uwanjani kama jibu la
msimamo ulioamuliwa na viongozi wa kanisa hili kwamba [sasa] wakati umefika wa kurudia
kusema tena na tena kilio kile cha, "TOKENI MIJINI."
WADHAMINI WA UCHAPISHAJIWA MAANDIKO YA ELLEN G. WHITE
YALIYOMO
Ukurasa
Wito wa Kuihama Miji............................................................. ............................
Kuikwepa Migogoro ya Vyama vya Wafanyakazi................................................
Ombi kwa Wazazi........................................................... ......................................
Kazi Katika Sehemu za Shamba........................................................... .................
Kujiandaa kwa Hatari Itakayoletwa na Amri ya Jumapili.....................................
Kujikusanya Watu Wengi katika Taasisi Zetu za Kazi..........................................
Kuongozwa kwa Maongozi ya Mungu............................................................ .......
Taasisi Zetu za Kazi Kuwa Mbali na Maeneo Yenye Msongamano wa Watu.......
Kukimbia Wakati wa Hali ya Hatari Pambano Litakapokuwa Linafikia Mwisho..
SEHEMU YA KWANZA
Wito wa Kuihama Miji
Hatari Kubwa Zilizomo Mijini
Niwachache wanaotambua umuhimu wa kukwepa, kwa kadiri iwezekanavyo, uhusiano wo wote
ule unaoleta uadui kwa maisha yetu ya kidini. Katika kuchagua mazingira yao, ni wachache mno
wanaoweka mawazoni mwao ufanisi wao wa kiroho katika nafasi ya kwanza.
Wazazina familia zao hukimbilia mijini, kwa sababu wanadhani kwamba ni rahisi kupata maisha
mazuri huko kuliko mashambani [vijijini]. Watoto wao, wakiwa hawana kazi yo yote ya kufanya
wasipokuwa shuleni kwao, hujipatia elimu ya mitaani. Kutoka kwa marafiki zao waovu
wanajifunza tabia za uovu na ubadhirifu [utumiaji mbaya wa fedha na vitu]. Wazazi huyaona hayo
yote, lakini itahitaji kujitolea mhanga kuweza kuyasahihisha makosa yao hayo, nao [wazazi]
huendelea kuishi mahali hapo walipo mpaka Shetani anawatawala watoto wao kabisa.
Niafadhali kujinyima mambo yote na kila tarajio la kidunia kuliko kuzihatirisha roho hizo za
thamani mlizokabidhiwa kuzitunza. Watashambuliwa vikali na majaribu, nao yapas a wafundishwe
jinsi ya kuyakabili; lakini ni wajibu wenu kuuondolea mbali kila mvuto, kulivunjilia mbali kila
zoea, kukata kila kifungo kinachowazuia msiwe na uhuru kamili, ulio wazi, na kujitoa wakf ninyi
wenyewe kwa moyo wenu wote pamoja na familia yenu kwa Mungu.
Badalaya msongamano wa watu uliomo mjini, tafuteni mahali fulani palipo kimya [pa upweke]
kwa kadiri iwezekanavyo, mahali palipo salama mbali na majaribu, nanyi mkiwa pale waleeni na
kuwaelimisha ili wapate kuwa watu wenye manufaa katika maisha yao. Nabii Ezekieli ndivyo
anavyoorodhesha sababu zilizoifanya Sodoma kutenda dhambi na kuangamizwa: "Kiburi, chakula
tele, na uvivu mwingi vilikuwa ndani yake pamoja na binti zake [vitongoji vyake]; wala haukuitia
nguvu mikono ya maskini na wahitaji." Wale wote wanaotaka kuokoka ili wasipatikane na
maangamizi kama yale ya Sodoma, hawana budi kuukwepa mwenendo ule ulioleta hukumu za
Mungu juu ya mji ule mwovu." ----- Testimonies, Gombo la 5, uk. 232,233 (1882).
Kuishi Mijini Sio Mpango wa Mungu
Ul imwenguni kote miji inageuka na kuwa mahali penye maovu mengi sana. Kila upande
huonekana mambo machafu na sauti za uovu. Kila mahali kuna vishawishi vya kuamsha ashiki
[tamaa mbaya ya uasherati] na ubadhirifu [matumizi mabaya ya mali na vitu]. Wimbi la ru shwa na
uhalifu linazidi kuumuka daima. Kila siku inayopita huleta taarifa za kutumia nguvu ----- ujambazi,
mauaji, kujiua, na uhalifu mwingine usiostahili hata kutajwa.
Maisha yaliyomo mijini sio maisha halisi, tena ni ya kinafiki. Tamaa kubwa sana ya kupata fedha,
mambo ya mpwitompwito [msisimko] yapitayo kasi pamoja na kutafuta anasa, kiu ya kuwakoga
[kujionyesha ufahari kwa] wengine, utajiri na ubadhirifu, mambo yote hayo ni nguvu ambazo, kwa
sehemu kubwa sana ya wanadamu, huyageuzia mawazo yao mbali na kusudi halisi la maisha yao.
Wanaufungua mlango wa kuingiza ndani yao maelfu ya maovu. Kwa vijana mambo hayo yana
nguvu nyingi ambayo karibu haizuiliki kabisa.
Mojawapoya majaribu yaliyojificha sana na ya hatari sana yanayowashambulia mno watoto na
v ijana katika miji ni kule kupenda anasa [starehe]. Sikukuu ni nyingi; michezo na mashindano ya
mbio za farasi huwavuta maelfu, na ule mpwitompwito upitao upesi pamoja na anasa huwavuta
kwenda mbali na majukumu mazito ya maisha yao. Fedha ambayo ingetunzwa kwa ajili ya
kuitumia kwa mambo mazuri zaidi hutapanywa ovyo katika burudani zao nyingi.
Kutokana na utendaji wa mashirika ya amana, na matokeo ya vyama vya wafanya kazi na migomo
yake, hali ya maisha mjini daima inakuwa ngumu zaidi na zaidi. Taabu kubwaziko mbele yetu; na
kwa familia nyingi kuondoka kwao kutoka mijini kutakuwa ni kwa lazima.
Mazingira ya nje katika miji mara nyingi ni ya hatari kubwa kwa afya. Uwezekano wa kudumu wa
kupatwa na magonjwa, kuenea kwa hewa chafu, maji machafu, chakula kilichochafuliwa, majengo
yaliyosongamana pamoja yenye giza na yasiyofaa kiafya, ni baadhi ya mambo mabaya ya
kukabiliana nayo humo.
Halikuwakusudi la Mungu kwamba watu waishi kwa kusongamana sana mijini, wakisongamana
pamoja katika mlolongo wa majumba katika kitalu kimoja na katika nyumba za kupangisha zenye
vyumba vingi. Hapo mwanzo aliwaweka wazazi wetu wale wa kwanza katikati ya madhari nzuri na
sauti nzuri. Anataka sisi tuifurahie siku ya leo. Kadiri tunavyokaribia sana kuwa katika hali ile
inayopatana na mpango wa Mungu wa awali, ndivyo kadiri tutakavyokuaa na nafasi nzuri zaidi ya
kujipatia afya ya mwili, akili, na roho. ----- The Ministry of Healing, uk. 363- 365. (1905)
Moyo wa Kusitasita
Sikuwezakulala baada ya kupita saa nane ya usiku mpakaasubuhi ya leo. Wakati wa usiku
nilikuwa natoa ushauri. Nilikuwa nazisihi baadhi ya familia kutumia njia alizoziweka Mungu, na
kuondoka mijini ili kuwaokoa watoto wao. Wengine walikuwa wanasitasita tu, bila kufanya juhudi
yo yote iliyo dhahiri.
Malaika wale wenye rehema walimharakisha Lutu na mkewe na binti zao kwa kuwashika mikono
yao. Lutu angekuwa ameharakisha kama Mungu alivyotaka, mke wake asingegeuka na kuwa nguzo
ya chumvi. Lutu alikuwa na roho hiyo ya kuchelewa- chelewa [kusitasita] mno. Hebu sisi na tusiwe
kama yeye. Sauti ile ile iliyomwonya Lutu kuondoka Sodoma inatuamuru sisi, ikisema, "Tokeni
kati yao, mkatengwe nao... Msiguse kitu kilicho kichafu." [2 Kor. 6:17.] Wale wanaolitii onyo hilo
watapata kimbilio. Hebu kila mwanaume na awe macho san a kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe,
tena ajaribu kuiokoa familia yake. Hebu na ajifunge kibwebwe [mkanda] kwa kazi hiyo. Mungu
ataonyesha hatua kwa hatua linalopaswa kufanywa baada ya hapo.
Isikilizeni sauti ya Mungu kupitia kwa mtume wake Paulo, isemayo: "Utimizeni wokovu wenu
kwa kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda
kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema" [Wafilipi 2:12,13]. Lutu akalikanyaga bonde lile
tambarare kwa hatua za kujilazimisha na kuchelewa - chel ewa tu. Kwa muda mrefu sana alikuwa
amezoeana na watenda maovu wale hata hakuweza kuiona hatari kubwa iliyomkabili mpaka hapo
mke wake aliposimama katika bonde lile akiwa nguzo ya chumvi milele." ----- Review and Herald,
Des. 11, 1900.
Miji Itapatilizwa kwa Hukumu za Mungu
Wakatiumekaribia ambapo miji mikubwa itapatilizwa kwa hukumu za Mungu. Katika kitambo
kidogo tu kilichobaki, miji hiyo itatikiswa vibaya mno. Haidhuru iwe mikubwa kiasi gani au
majengo yake yawe imara jinsi gani, haidhuru vifaa vya kujihami na moto viwe vimeandaliwa kwa
wingi namna gani, acha Mungu ayaguse majengo hayo, katika muda wa dakika chache tu au saa
chache yatakuwa yameharibiwa kabisa na kuwa magofu.
Mijihiyo miovu [isiyomcha Mungu] itafagiliwa mbali kwa fagio la maangamizi. Katika uharibifu
unaoyapata majengo makubwa na sehemu kubwa za miji hivi sasa, Mungu anatuonyesha kile
kitakachoiangukia dunia yote. ----- Testimonies, Gombo la 7, uk. 82,83. (1902).
Matokeo ya Maonyo Yaliyopuuzwa
Nimeagizwakutangaza ujumbe huu kuwa miji ile iliyojaa maasi [uvunjaji wa sheria], na ile iliyo
miovu kupita kiasi, itaharibiwa kwa matetemeko, kwa moto, na kwa mafuriko. Dunia yote
itaonywa na kujua kwamba yuko Mungu atakayedhihirisha mamlaka yake kama Mungu. Mawakala
[wajumbe] wake wasioonekana kwa macho [malaika] watasababisha maangamizi, kuteketeza kwa
moto, na vifo. Utajiri wote uliolundikwa utakuwa kama si kitu....
Maafayatakuja ----- yaani, maafa ya kuogofya mno, yasiyotarajiwa kabisa; na maangamizi hayo
yatafuatana moja baada ya jingine. Kama watu watayasikia [watayatendea kazi] maonyo haya
ambayo Mungu ametoa, na iwapo makanisa yatatubu, na kurudia utii wao [kwa Mungu], basi, miji
mingine itaachwa isiharibiwe kwa muda fulani. Lakini endapo watu waliodanganyika wataendelea
kutembea katika njia ile ile walimokuwa wakitembea, wakiendelea kuidharau Sheria ya Mungu
[Amri Kumi], na kuhubiri [mafundisho ya] uongo mbele ya watu, basi, Mungu ataruhusu majanga
yawapate ili akili zao zipate kuamshwa.
Bwanahatawatupilia mbali kwa ghafula wale wote wanaozivunja amri zake [kumi], wala
kuyaangamiza mataifa mazima; lakini ataiadhibu miji na mahali pale ambapo watu wamejitoa
kabisa kutawaliwa na nguvu za kishetani. Kwa ukali sana miji ya mataifa itashughulikiwa, hata
hivyo haitapatilizwa kwa ghadhabu kali mno ya Mungu, kwa sababu baadhi ya watu waliomo
humo watajinasua kutoka katika madanganyo hayo ya yule adui [Shetani], kisha watatubu na
kuongolewa, na wakati uo huo watu wengi sana watakuwa wanajiwekea akiba ya ghadhabu kwa
siku ile yaghadhabu [ya Mwana- Kondoo, yaani, Kristo]. [Ufunuo 6:14- 17; 15:1; 16:1- 21.] -----Evangelism, uk. 27. (1906)
Ukaribu Sana wa Kuja kwa Hukumu za Mungu
Ziposababu kwa nini sisi tusijenge [nyumba zetu] mijini. Juu ya miji hii, hukumu za Mungu zi
kari bu sana kuiangukia. ----- Letter 158, 1902.
Laitikama watu wa Mungu wangeyajua maangamizi yaliyo karibu sana kuja juu ya maelfu ya
miji, ambayo kwa sasa imejisalimisha kabisa kuabudu sanamu [Kol. 3:5,6; Efe. 5:5- 7; Kut. 20:4- 6].
----- Review and Herald,Sept. 10, 1903.
Maono ya Maangamizi Makubwa
AlfajiriIjumaa iliyopita, kabla tu sijaamka usingizini, mandhari [picha] iliyonigusa sana moyoni
ilionyeshwa mbele yangu. Nikajiona kana kwamba nimeamka usingizini, ila sikuwa nyumbani
mwangu. Kupitia katika madirisha niliweza kuona moto mkubwa wa kutisha uliokuwa
unayateketeza majumba. Mipira mikubwa ya moto [huenda ikawa ni mabomu] ilikuwa ikidondoka
juu ya nyumba zile, na kutoka katika mipira hiyo mishale ya moto ilikuwa inaruka kuelekea kila
upande.Ilikuwa haiwezekani kabisa kuizuia mioto hiyo iliyokuwa imewashwa, tena mahali pengi
palikuwa panaharibiwa. Hofu kuu iliyowashika watu ilikuwa haielezeki. ----- Evangelism, uk. 29.
(1900)
Juhudi za Mungu za Kuwaamsha Watu
Nikiwabado ningali pale Loma Linda, California, Aprili 16, 1906, maono ya ajabu sana yalipita
mbele yangu. Wakati wa njozi zangu za usiku, nalikuwa nimesimama kwenye mwinuko [kilima],
kutoka hapo niliweza kuziona nyumba zikitikiswa kama tete katika upepo. Majengo, makubwa kwa
madogo, yalikuwa yakianguka chini. Majumba ya anasa wanayoyatembelea watu wengi, nyumba
za michezo ya kuigiza, hoteli, na nyumba za matajiri zilitikiswa na kuharibiwa kabisa. Maisha
mengi yakafutiliwa mbali, na anga ilikuwa imejaa sauti za vilio vikubwa kutokana na wale
waliokuwa wamejeruhiwa na kuogofywa sana.
Malaikawa Mungu waangamizao walikuwa wanafanya kazi yao. Mguso mmoja tu, majengo
yaliyojengwa imara sana ambayo watu walifikiri kwamba yalikuwa salama kutokana na hatari ya
kila namna, kwa ghafula yakawa malundo ya takataka. Hapakuwa na hakika ya kuwa na usalama
mahali po pote pale. Mimi sikujiona kuwa nimo katika hatari yo yote maalum, lakini utisho mkuu
wa matukio yale yaliyopita mbele yangu mimi siwezi kupata maneno ya kuelezea. Ilionekana kana
kwamba uvumilivu wa Mungu ulikuwa umefikia kikomo chake kabisa, na ya kwamba siku ile ya
hukumu ilikuwa imekuja.
Malaikayule aliyekuwa amesimama kando yangu ndipo akanipasha habari kwamba ni wachache
tu waliokuwa na wazo lo lote kuhusu uovu uliomo katika u limwengu wetu hivi leo, na hasa uovu
ule ulio katika miji mikubwa. Akatangaza kwamba utawala wa Mungu ulio mkuu kuliko wote, na
utakatifu wa Sheria yake [Amri Kumi], havina budi kufunuliwa kwa wale wanaoendelea kukataa
kutoa utii wao kwa Mfalme huyo wa waf alme. Wale wanaochagua kubaki katika hali yao ya uasi
[kuvunja Amri zake Kumi], ni lazima wapatilizwe kwa hukumu kwa rehema [zake Mungu], ili,
kama ikiwezekana, wapate kuamshwa [kuzinduliwa] watambue uovu wa njia yao. -----Testimonies, Gombo la 9, uk. 92,93. (1909)
Hatari Itakayowakabili Watakaoendelea Kubaki Mjini Bila Sababu
Kulinganana nuru ile niliyopewa, mimi nawasihi watu kutoka na kuvihama vituo vikubwa
vilivyojaa watu wengi. Miji yetu inazidi kuwa miovu, tena, inaonekana wazi zaidi na zaidi ya
kwamba wale watakaobaki ndani ya miji hiyo bila sababu [ulazima wo wote] watafanya hivyo kwa
athari kubwa ya wokovu wa nafsi zao. ----- Manuscript 115, 1907.
SEHEMU YA PILI
Kuikwepa Migogoro ya Kazi
Ondokeni [Mijini] Kwenda Vijijini Kwenye Uhuru
Wakatiunaharakisha sana kuja ambapo uongozi wa Vyama vya Wafanyakazi utatumia uwezo
wake kuleta mateso mengi kwa watu. Tena na tena Bwana ameniagiza kwamba watu wetu watoke
mijini pamoja na familia zao kwenda vijijini, ambako wanaweza kujipatia chakula chao wenyewe;
kwa maana siku zijazo tatizo la kununua na kuuza litakuwa zito sana. Hivi sasa tungeanza kuyatii
maagizo hayo yaliyotolewa kwetu tena na tena. Tokeni mijini kwenda kwenye maeneo ya shamba
[vijijini], ambako nyumba hazijasongamana sanamahali pamoja, na ambako mtakuwa huru mbali
na usumbufu utakaoletwa na wale adui zetu. ----- Letter 5, 1904.
Iepukeni Migongano Iletwayo na Vyama
Watuwamejiunga katika mashirika yenye kusudi baya ili kumpinga Bwana wa majeshi. Mashirika
hayo yenyekusudi baya yataendelea kuwapo mpaka hapo Kristo atakapoondoka mahali pake pa
maombezi mbele ya kiti kile cha neema, na kuvaa mavazi yake ya kulipiza kisasi [Ufu. 19:11- 16].
Mawakala [wajumbe] wa Shetani wamo katika kila mji, wanashughulika sana kuwakusan ya katika
vyama wale wote wanaoipinga Sheria ya Mungu [Amri Kumi]. Wale wanaodai kuwa ni watakatifu
na wale wanaosema waziwazi kuwa wao ni waumini wanachagua na kusimama upande wa vyama
hivyo. Huu sio wakati wa kuwa dhaifu kwa watu wa Mungu. Hatuwezi kumudu kukaa bila kukesha
[kuwa macho] hata kwa dakika moja. ----- Testimonies, Gombo la 8, uk. 42. (1904).
Dhiki Itakayoletwa na Vyama vya Matajiri I Mbele Yetu
Vyamavya Matajiri [Waajiri] vitakuwa ni njia mojawapo itakayoleta duniani wakati wa taabu
ambao haujapata kuwako [kuonekana] tangu mwanzo wa dunia hii. ----- Letter 200, 1903.
Migogoro Kati ya Mashirikisho ya Matajiri na Vyama vya Wafanyakazi
Kaziwanayopaswa kufanya watu wa Mungu ni kujiandaa kwa matukio yale ya siku zijazo,
ambayo yatawajia ghafula kwa nguvu nyingi. Ulimwenguni humu mashirika makubwa sana yenye
ukiritimba [yanayomiliki na kuhodhi mali nyingi] yataundwa. Watu watajifunga wenyewe kwa
mikataba katika vyama mbalimbali ambavyo vitawafungia katika mazizi ya yule adui. Watu
wachache watajiunga pamoja na kuishika kwa nguvu mali yote iliyopatikana katika mikondo fulani
ya biashara. Vyama vya Matajiri [Waajiri] vitaundwa, na wale wote wanaokataa kujiunga na
vyama hivyo watakuwa watu wanaoangaliwa kwa jicho baya sana. ----- Letter 26, 1903.
Kujiandaa kwa Tukio Hilo
Vyamavya Matajiri na mashirikisho ya ulimwengu huu yenye kusudi baya ni mtego kwetu.
Achana nayo, na kwenda mbali nayo, enyi ndugu zangu. Msishirikiane nayo kabisa. Kwa sababu
kwa ajili ya vyama hivyo na mashiri kisho hayo yenye kusudi baya, muda si mrefu itakuwa vigumu
sana kwa taasisi zetu kutekeleza kazi zake mijini. Onyo langu ni hili: Ondokeni mijini. Msijenge
hospitali zetu zo zote mijini. Waelimisheni watu wetu watoke mijini kwenda mashambani [vijijini],
am bako wataweza kujipatia sehemu ndogo ya ardhi, na kujijengea makazi yao wenyewe pamoja na
watoto wao....
Migahawayetu haina budi kuwekwa mijini; maana vinginevyo watumishi wa migahawa hiyo
wasingeweza kuwafikia watu na kuwafundisha kanuni za maisha bora. Na kwa wakati huu tutakalia
nyumba za mikutano [makanisa] zilizomo mijini. Lakini kabla ya muda mrefu kupita kutakuwa na
vita na machafuko mijini ya aina ambayo wale watakaotamani kuihama [miji] hawataweza kufanya
hivyo. Yatupasa tuwe tunajiandaa [sasa] kukabiliana na matatizo hayo. Hii ndiyo nuru niliyopewa
mimi. ----- General Conference Bulletin, Aprili 6, 1903.
Kuuhifadhi Utu Wetu
Kwa miaka mingi nimepewa nuru ya pekee kwamba hatupaswi kuweka makao makuu ya kazi yetu
mijini. Misukosuko na machaf uko yanayoijaza miji hiyo, hali zile zitakazoletwa na Vyama vya
Wafanyakazi na migomo yao, itakuwa kizuizi kikubwa kwa kazi yetu. Watu wanajaribu kuwafunga
chini ya vyama fulani wale wote wanaofanya kazi mbalimbali. Huo sio mpango wa Mungu, bali ni
mpango wa mamlaka ambayo kwa vyo vyote vile tusingekubaliana nayo. Neno la Mungu
linaendelea kutimia; waovu wanajifunga wenyewe katika matita matita tayari kuchomwa moto.
Hivi sasa yatupasa kutumia uwezo wote tuliopewa [na Mungu] katika kuutoa ujumbe wa onyo la
mwisho kwa ulimwengu mzima. Katika kazi hii hatuna budi kuuhifadhi utu wetu. Hatupaswi
kujiunga na vyama vya siri au na vyama vya matajiri na vya wafanyakazi. Tunatakiwa kusimama
huru ndani ya Mungu, daima tukiwa tunamtazama Kristo kwa maagizo yake. Kuham a kwetu kote
kutoka mahali fulani kwenda mahali pengine kufanyike kwa kuzingatia umuhimu wa kazi
inayotakiwa kutimizwa kwa ajili ya Mungu wetu. ----- Testimonies, Gombo la 7, uk. 84. (1902)
Kuidharau Sheria ile ya Amri Kumi
Vyamahivyo ni mojawapo y a dalili za siku za mwisho [Yakobo 5:1- 6]. Watu wanajifunga
wenyewe katika matita matita tayari kuchomwa moto. Pengine hao ni washiriki wa kanisa, lakini
wanapojiunga na vyama hivyo, hakuna uwezekano kwao wa kutunza amri [kumi] za Mungu; kwa
maana kule kujiunga na vyama hivyo maana yake ni kuidharau kabisa Sheria ile ya Amri Kumi.
"Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako
zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako" [Luka 10:27]. Maneno hayo
yan aweka jumla ya wajibu wote umpasao mwanadamu. Yana maana ya kuutoa wakf mwili wote,
yaani, mwili, roho, na nafsi, kwa kazi ya Mungu. Watu wanawezaje kuyatii maneno hayo, na
wakati uo huo kujifunga wenyewe kwa kiapo cha kukisaidia [chama] kile kinachowanyima uhuru
wa kufanya mambo yao majirani zao? Tena, inawezekanaje kwa watu kuyatii maneno hayo, na
kuyaunda mashirika yanayowadhulumu watu maskini haki zao ambazo wanastahili kupata,
yakiwazuia wasinunue wala wasiuze isipokuwa kwa masharti fulani yaliyowekwa? ----- Letter 26,
1903.
Vyama Vinavyoundwa au Vile Vitakavyoundwa
Walewanaodai kuwa ni watoto wa Mungu kwa vyo vyote vile hawatakiwi kujifungamanisha na
vyama vya wafanyakazi vinavyoundwa au vile vitakavyoundwa [baadaye]. Jambo hilo Bwana
anakataza. Je! wale wanaojifunza unabii hawawezi kuona na kuelewa yale yaliyo mbele yetu? -----Letter 201, 1902.
SEHEMU YA TATU
Ombi Kwa Wazazi
Waondoeni Watoto Wenu Mbali na Mahali Penye Maovu
Faidayo yote ipatikanayo kutokana na shughuli za kila siku za maisha haya isiruhusiwe
kuwashawishi wazazi kuacha kuwalea watoto wao. Kila inapowezekana, ni wajibu wa wazazi
kujenga makao yao mashambani [vijijini] kwa ajili ya watoto wao. Watoto na vijana wanapaswa
kulindwa kwa uangalifu. Wangeondolewa na kupelekwa mbali na mahali penye maovu mengi
ambapo panapatikana katika miji yetu. Hebu na wazungushiwe mivuto ile inayopatikana katika
nyumba ya kweli ya Kikristo ----- yaani, nyumba ile anamokaa Kr isto. ----- Letter 268, 1906.
Kabla Pigo Lile Halijafurika
Kablapigo lile halijafurika juu ya wakazi wa dunia hii, Bwana anawaagiza wale walio Waisraeli
kweli kweli kujiweka tayari kwa tukio lile. Kwa wazazi anawapelekea kilio cha onyo, akisema,
Wakusanyeni watoto wenu na kuwaleta nyumbani mwenu; wakusanyeni na kuwatenga mbali na
wale wanaozidharau amri [kumi] za Mungu, yaani, wale wanaofundisha watu uovu na kutenda
uovu. Tokeni nje ya miji mikubwa haraka iwezekanavyo. Jengeni shule zinazoendeshwa n a kanisa.
Wapeni watoto wenu Neno la Mungu kama msingi wa elimu yao yote. ----- Testimonies, Gombo la
6, uk. 195.
Nimeagizwana Bwana niwaonye watu wetu wasikimbilie kwa wingi mijini ili kujijengea makazi
humo kwa ajili ya familia zao. Kwa akina baba na akina mama nimeagizwa kusema maneno haya,
Msikose kuwatunza watoto wenu ili wabaki ndani ya maeneo ya nyumba na viwanja vyenu. -----Manuscript 81, 1900.
Roho za Watoto Wenu au Maisha Rahisi na Starehe Zenu
Ninyimsiendelee tena kuwaweka watoto wenumahali pale watakapokabiliana na majaribu
yaliyomo mijini, miji ambayo imefikia kilele chake cha kuangamizwa. Bwana ametuma onyo lake
kwetu pamoja na ushauri wake ili tutoke mijini. Basi na tusiendelee kuweka vitega uchumi zaidi
katika miji hiyo. Akina baba na mama, mnazifikiriaje roho za watoto wenu? Je! mnawatayarisha
waliomo nyumbani mwenu kwa kunyakuliwa kwenda katika majumba yale ya kifalme kule
mbinguni? Je! mnawaandaa hao kuwa miongoni mwa familia ile ya kifalme? yaani, watoto wa
Mfalme yule wa mbinguni? "Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata
hasara ya nafsi yake?" [Mathayo 16:26.] Mtalinganishaje maisha rahisi, starehe,hali ile yenye
manufaa isiyo na wasiwasi [iliyomo humo mijini] na thamani ya roho za watoto wenu? -----Manuscript 76, 1905.
Tabia za Kikristo Zinajengeka Vizuri Zaidi Katika Maeneo ya Upweke
Hakunahata familia moja katika mia ambayo ikiendelea kukaa mjini itakuwa na maendeleo
mazuri kimwili, kiakili, au kiroho. Imani, tumaini, upendo, furaha, vinaweza kupatikana kwa vizuri
zaidi katika mahali pa upweke, ambapo pana mashamba na vilima na miti. Nendeni na watoto
wenu mbali na mambo yale yanayoonekana waziwazi [tamasha] na sauti za mjini, mbali na
makelele ya magari yanayopita mitaani pamoja na makundi ya watu, hapo ndipo akili zao [watoto
wenu] zitakuwa na afya zaidi. Itaonekana kuwa ni rahisi zaidi kwao kuikumbuka mioyoni mwao
kweli ile ya Neno la Mungu. ----- Manuscript 76, 1905.
Wapelekeniwatoto wenu kwenye shule zile zilizomo mjini, ambako kila aina ya majaribu
huwangojea ili kuwatamanisha na kuwadhalilisha, ndipo kazi ile ya kujenga tabia itakuwa ngumu
mara kumi kwa pande zote mbili, yaani, kwa wazazi na kwa watoto. ----- Fundamentals of
Christian Education, uk. 326. (1894)
Kimbilio Katika Maeneo ya Mashambani
Wazazi na waelewe ya kwamba malezi ya watoto wao ni kazi ya maana katika kuziokoa roho zao.
Katika maeneo yale ya mashambani [vijijini] mazoezi ya viungo mengi ya kufanya yenye manufaa
[kiafya] yatapatikana kwa kufanya mambo yale yan ayopaswa kufanywa, ambayo yatawapa afya ya
kimwili kwa kuzikuza neva zao na misuli. Tokeni mijini, huo ndio ujumbe wangu kwa ajili ya
kuwalea watoto wetu katika maadili mema.
Mungualiwapa wazazi wetu wale wa kwanza njia ya elimu ya kweli alipowaagiza ku ilima ardhi
na kuyatunza makao yao katika Bustani ile. Baada ya dhambi kuingia, kutokana na utovu wao wa
utii kwa matakwa yake Bwana, kazi iliyofanyika kuilima ardhi ikawa imeongezeka sana, maana
nchi, kutokana na laana ile, ikazaa magugu na michongoma. Lakini kazi ile yenyewe haikutolewa
kwao kwa sababu ya dhambi. Bwana Mkuu Mwenyewe akaibarikia kazi ile ya kuilima ardhi.
"KAMA VILE ILIVYOKUWA ... SIKU ZA NUHU"
Nikusudi lake Shetani kuwashawishi wanaume na wanawake kwenda mijini, isitoshe, ili kufikia
lengo lake anavumbua kila namna ya mambo mapya [mitindo mipya] na burudani, kila aina ya
mambo ya kusisimua. Na miji ya ulimwengu wa leo inageuka na kuwa kama ilivyokuwa miji ile
kabla ya Gharika.
Daimatungebeba mzigo huo [wa kujihadhari] tunapoyaon a maneno hayo ya Kristo yakitimia,
"Kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu."
Mathayo 24:37. Katika siku zile kabla ya Gharika, kila aina ya burudani ilibuniwa ili kuwafanya
wanaume na wanawake kuwa na usahaulifu [wa mambo ya Mungu] na kutenda dhambi. Leo hii,
mwaka huu wa 1908, Shetani anafanya kazi yake kwa nguvu nyingi, ili hali zile zile zipate kuwapo.
Nao ulimwengu unazidi kuwa mwovu. Uhuru wa dini hautaheshimiwa sana na wale wanaojiita
Wakristo, kwa kuwa wengiwao hawayajui kabisa mambo ya kiroho.
Hatuwezikushindwa kuona ya kwamba mwisho wa ulimwengu huu karibu sana unakuja. Shetani
anafanya kazi yake katika mioyo [mawazo] ya wanaume na wanawake, na wengi wanaonekana
kana kwamba wamejazwa na tamaa ya kupata burudani na misisimko. Kama vile ilivyokuwa katika
siku zile za Nuhu, kila aina ya uovu inazidi kuongezeka. Kwa wakati kama huu, watu wale
wanaojaribu kuzishika amri [kumi] za Mungu wangetafuta mahali pa upweke [pa kuishi] mbali na
miji hiyo....
SI HASA RA KWENU
Ninani basi atakayeonywa? Tunarudia tena kusema, Tokeni Mijini. Msidhani kwamba ni hasara
kubwa sana kwenu, kwamba ni lazima kwenda vilimani na milimani, bali tafuteni mahali pale pa
upweke [ukimya] ambapo mnaweza kuwa na Mungu peke yenu, mki jifunza mapenzi yake na njia
yake....
Ninawasihiwatu wetu kuifanya iwe ndiyo kazi yao ya maisha kutafuta maisha yao ya kiroho.
Kristo yu mlangoni. Hii ndiyo maana nawaambia watu wetu, Msifikirie ya kuwa ni taabu
mnapoitwa kuiacha miji na kuhamia katika maeneo ya shamba [vijijini]. Huko mibaraka mingi
inawangojea wale watakaoishikilia. Kwa kuziangalia mandhari zile [sura za nchi] za maumbile,
yaani, kazi ile ya Muumbaji, kwa kujifunza kazi ya mikono yake [uumbaji wake] Mungu, bila
kujitambua mtabadilishwana kufanana naye. ----- Manuscript 85, 1908.
Kujipatia Matunda Bora Kabisa ya Maisha Haya
Jengola gharama nyingi, fanicha iliyonakishiwa sana, mapambo, anasa, na raha, mambo hayo
hayaleti hali zile zilizo za muhimu kwa maisha ya furaha, yenye manu faa. Yesu alikuja hapa
duniani kufanya kazi kubwa sana iliyopata kufanywa miongoni mwa wanadamu. Alikuja kama
balozi [mjumbe] wa Mungu, kutuonyesha sisi jinsi ya kuishi ili tuweze kujipatia matunda bora
kabisa ya maisha haya. Ni hali [mazingira] gani basi zilizochaguliwa na Baba yetu wa milele kwa
ajili ya Mwanawe? Ni nyumba ile iliyokaa mahali pale pa upweke [kimya] katika vilima vile vya
Galilaya; nyumba iliyopata mahitaji yake kwa kazi ya uaminifu, yenye heshima; maisha yale ya
kawaida; kupambana kila si ku na matatizo pamoja na shida; kujikana nafsi, matumizi mazuri ya
kipato chao, na huduma yao iliyotolewa kwa moyo wa uvumilivu na furaha; saa ile ya kujifunza
kando ya mama yake, wakiwa na gombo la Maandiko lililofunguliwa wazi; macheo yale tulivu au
utusitusi ule wa asubuhi katika bonde lile la majani mabichi; huduma takatifu ya maumbile yale;
kujifunza uumbaji na maongozi ya Mungu; na moyo wake kuwasiliana na Mungu, ----- hizo
zilikuwa ndizo hali [mazingira] na nafasi nzuri za maisha ya mwanzo ya Yesu.
WAKUU NI URITHI UTOKANAO NA MAISHA YA SHAMBA
Hivyo ndivyo ilivyo kwa sehemu kubwa ya watu walio bora na wakuu katika vizazi vyote. Someni
historia ya Ibrahimu, Yakobo, na Yusufu, na ya Musa, Daudi, na Elisha. Jifunzeni maisha ya watu
wa nyakati zilizofuata baadaye waliostahili kabisa kuzijaza nafasi zile za amana na madaraka, watu
ambao mvuto wao umekuwa na mafanikio makubwa sana katika kuuinua juu ulimwengu huu.
Niwangapi miongoni mwa hao walilelewa katika makazi ya mashambani [vijijini]. Hawakuijua
anasa hata kidogo. Hawakuutumia ujana wao katika burudani. Wengi walilazimika kupigana na
umaskini na shida. Walijifunza mapema kufanya kazi [kwa mikono yao], na maisha yao ya
kujishughulisha sana katika maeneo yale yaliyo wazi yaliwapa nguvu za kimwili na kupanuka kwa
uwezo wao kiakili. Wakiwa wamelazimika kutegemea rasilimali [nyenzo] zile walizokuwa nazo,
walijifunza kupambana na shida na kuvishinda vipingamizi, tena walijipatia ujasiri na uvumilivu.
Walijifunza masomo ya kujitegemea na kujitawala naf si zao. Wakiwa wamekingwa kwa kiwango
kikubwa mbali na marafiki wabaya, walitosheka na furaha za kawaida na urafiki mzuri ujengao.
Katika uchu wao wa chakula walifuata chakula cha kawaida na kuwa na kiasi katika mazoea yao.
Walitawaliwa na kanuni, tena wal ikua wakiwa safi [wakiwa na mwenendo mzuri], wakiwa na
nguvu na unyofu wa moyo. Walipotakiwa kufanya kazi zao za maisha, walikwenda wakiwa na
nguvu za kimwili na kiakili, wakiwa na moyo uliochangamka, na uwezo wa kupanga mipango na
kuitekeleza, tena wakiwana uthabiti wa kuyapinga maovu, mambo ambayo yaliwafanya kuwa na
uwezo dhahiri wa kutenda mema ulimwenguni.
BORA KULIKO UTAJIRI
Borakuliko urithi mwingine wo wote mnaoweza kuwapa watoto wenu itakuwa ni zawadi ile
mtakayowapa ya mwili wenye afya, akili timamu, na tabia nzuri. Wale wanaojua kile kinacholeta
ufanisi wa kweli katika maisha haya mara nyingine watakuwa na busara. Wataweka mbele yao
mambo yale yaliyo bora kwa namna watakavyochagua makazi yao.
Badalaya kuishi mahali pale ambapo kazi za wanadamu zinaweza kuonekana waziwazi, penye
tamasha na sauti zinazoamsha mawazo machafu, mahali pale ambapo misukosuko na ghasia huleta
uchovu na wasiwasi, nendeni mahali ambako mnaweza kuangalia kazi za [uumbaji wa] Mungu.
Jipatieni pumziko la nafsi zenu katika uzuri na utulivu na amani ya maumbile [viumbe vya asili].
Jicho lenu na liangalie mashamba ya chanikiwiti, vijisitu, pamoja na vilima. Angalieni mbingu ile
ya samawi, isiyozuiwa na vumbi na moshi wa mjini hata isiweze kuonekana, vuteni hewa ile ya
m binguni inayowatia nguvu. Mbali na mambo yale yaliyomo mjini yanayovuta mawazo yenu na
kuyatawanya, nendeni pale mnapoweza kukaa kirafiki na watoto wenu, mnapoweza kuwafundisha
ili wapate kujifunza habari za Mungu kwa njia ya kazi zake [uumbaji wake], na kuwalea ili wawe
na maisha ya unyofu na yenye manufaa [kwao wenyewe na kwa wengine]. ----- The Ministry of
Healing, uk. 265- 267. (1905)
Faida Nyingi za Shughuli Zinazofanyika Nje
Lingekuwani jambo jema kwenu kuweka kando masumbufu yenu yanayowafadhaisha, na kupata
mahali pa faragha huko shamba [vijijini], ambako hakuna mvuto wenye nguvu wa kuyaharibu
maadili ya watoto na vijana wenu.
Nikweli, hamtaweza kuondokana kabisa na maudhi yote pamoja na masumbufu yanayofadhaisha;
lakini kule mgeweza kuyaep uka maovu mengi na kufunga mlango dhidi ya gharika ya majaribu
yanayotishia kuyatawala kabisa mawazo ya watoto wenu. Wanahitaji kazi ya kufanya na mambo
mbalimbali tofauti ya kushughulika nayo. Mambo ya jinsi ile ile waliyozoea kufanya nyumbani
mwenu huwaf anya wasiwe na raha [huwakinai], na kuwa watukutu, kisha wanajiingiza katika tabia
ile ya kujichanganya pamoja na vijana wale waovu wa mjini, hivyo hujipatia elimu ya mitaani
huko....
Kuishihuko shamba [vijijini] kungewaletea [watoto na vijana] manufaa mengi sana; maisha yao
ya shughuli nyingi nje ya nyumba yangekuza afya yao kiakili na kimwili. Wawe na bustani ya
kupalilia, ambamo watapata furaha na kazi yenye manufaa kwao. Kuitunza mimea na maua kuna
mwelekeo wa kukuza akili za kupambanua mema na mabay a pamoja na kuwa na busara, na wakati
uo huo ufahamu wao kuhusu uumbaji mzuri na wenye manufaa wa Mungu una mvuto kwao
unaowabadilisha na kuwafanya wawe waungwana katika mawazo yao, wakiuhusisha [uumbaji
huo] na Muumbaji na Bwana huyo wa vyote. ----- Testi monies, Gombo la 4, uk. 136. (1876)
Tusitazamie Mwujiza Wo Wote Kuigeuza Njia Yetu Mbaya
Nayaangaliamaua haya, na kila wakati ninapoyaangalia nafikiria juu ya Edeni. Hayo yanaonyesha
upendo wa Mungu alio nao kwetu. Hivyo anatupatia sisi katika dunia hii mwonjo mdogo tu wa
Edeni ile. Anatutaka sisi kufurahia vitu vizuri alivyoviumba, na ndani yake kuona sura [picha] ya
kile anachotaka kutufanyia sisi.
Anatutakasisi kuishi mahali pale palipo na nafasi tele. Watu wake hawatakiwi kusongamana
mijini. Anawataka waende na familia zao nje ya miji, ili wapate kujiandaa vizuri kwa ajili ya uzima
ule wa milele. Kitambo kidogo [kilichobaki] watalazimika kuondoka mijini.
Miji hiyo imejaa uovu wa kila namna, ----- pamoja na migomo na mauaji na watu kujiua wen yewe.
Shetani yu ndani yake [miji hiyo], akiwaongoza watu katika kazi yao ya maangamizi. Chini ya
mvuto wake wanaua kwa sababu tu ya kuua, na kitendo hicho wataendelea zaidi na zaidi kufanya....
Tukijiwekawenyewe chini ya mivuto ile mibaya iliyokatazwa,je! tutazamie kwamba Mungu
atafanya mwujiza wo wote wa kuigeuza njia yetu hiyo mbaya? ----- La, hasha. Tokeni mijini
haraka iwezekanavyo, na kununua sehemu ndogo ya ardhi [vijijini], ambako mnaweza kuwa na
bustani, mahali ambako watoto wenu wanaweza kuyaangalia maua yakuapo, na kujifunza kwayo
mafunzo ya kuwa na maisha ya kawaida na usafi wa moyo. ----- General Conference Bulletin,
Machi 30, 1903.
SEHEMU YA NNE
Kazi Mbalimbali Katika Maeneo ya Vijijini
Ardhi Itupatie Mahitaji Yetu
Kwamibaraka yake Mungu, ardhi hii ikilimwa itatupatia mahitaji yetu. Tusikate tamaa kwa
mambo ya maisha haya kwa sababu ya kuonekana hali ile ya kushindwa, wala tusivunjike moyo
kwa kuchelewa mambo. Yatupasa kuulima udongo kwa f uraha, matumaini, na shukrani, tukisadiki
ya kwamba ndani ya udongo huo kuna hazina nyingi za kuweka ghalani mwetu kwa mfanyakazi
mwaminifu, yaani, hazina zile zenye utajiri mwingi kuliko dhahabu na fedha. Shutuma ile
inayotolewa kwake [huo udongo] kuwa ni mnyimivu [hautupatii mavuno ya kutosha] ni ya uongo.
Kwa kuilima vizuri na kutumia akili ardhi itatoa hazina zake [mazao] kwa manufaa ya
mwanadamu. Milima na vilima hubadilika; dunia huchakaa kama vazi kuukuu; lakini mbaraka wa
Mungu, unaoandaa meza [chakula] jangwani kwa ajili ya watu wake, hautakoma kamwe.
Nyakatingumu sana zi mbele yetu, tena ipo haja kubwa kwa familia kutoka mijini kwenda kule
shamba [vijijini], kweli yaweza kupelekwa katika vichochoro sawasawa tu na vile inavyoweza
kupelekwa katikanjia kuu za usafiri za dunia hii. Mengi hutegemea juu ya kupanga mipango yetu
kulingana na Neno la Bwana, na kwa juhudi ya kudumu kuitekeleza [mipango hiyo]. Mambo
mengi sana hutegemea bidii yetu iliyotolewa wakf pamoja na ustahimilivu wetu kuliko kutegem ea
akili nyingi isiyo ya kawaida na maarifa yale yapatikanayo katika vitabu ambayo hayatendewi kazi.
Talanta zote na uwezo wote aliowapa mawakala wake wa kibinadamu, visipotumika, basi, havina
faida yo yote kwetu.
Kuzirudianjia zile rahisi [za utendaji kazi] kutathaminiwa na watoto na vijana wetu. Kazi ya
bustanini na shambani italeta badiliko linalokubalika badala ya kawaida zile zinazochosha sana za
masomo ya kinadharia, ambayo akili za watoto wao wadogo zisingejihusisha nayo kwa muda
mrefu. Kwa mtoto mdogo aliye dhaifu kiakili, ambaye anaona masomo ya vitabuni kuwa
yanamchosha sana, na kwake huwa ni vigumu kuyakumbuka, kazi kama hiyo itakuwa na manufaa
ya pekee kwake. Kuna afya na furaha kwa ajili yake katika kujifunza maumbile [viumbe vya asili];
na picha inayozama moyoni mwake haitaweza kufifia, kwa maana mambo hayo yatahusishwa na
vitu vile vilivyo mbele ya macho yake daima. ----- Testimonies, Gombo la 6, uk. 178,179. (1900)
Mkiwa na Kipande Kidogo cha Ardhi na Nyumba Nzuri ya Kuishi
Ardhiinapaswa kushughulikiwa mpaka iweze kutoa nguvu yake; lakini pasipo kuwapo mbaraka
wa Mungu haiwezi kutoa kitu. Hapo mwanzo, Mungu aliangalia vyote alivyoviumba, na kusema
kwamba vilikuwa vyema sana. Laana ililetwa juu ya nchi [udongo] kama matokeo ya dhambi.
Lakini, je! laana hiyo izidi kuongezeka kwa kuzidi kufanya dhambi? Ujinga unaendelea kuleta
matokeo yake yanayoleta madhara mengi. Watumishi walegevu [wavivu] wanazidisha maovu kwa
tabia zao za kivivu. Wengi hawako tayari kujipatia chakula chao kwa jasho la uso wao, wanakataa
kuilima ardhi. Lakini ardhi inazo hazina zake zilizojificha chini kwa ajili ya wale walio na ujasiri
na nia na uvumilivu wa kuzikusanya hazina zake hizo. Akina baba na mama walio na kipande cha
ardhi na nyumba nzuri ya kuishi, hao ni wafalme na malkia.
Wakulimawengi wameshindwa kupata mavuno ya kutosha kutoka katika mashamba yao kwa
sababu wameichukulia kazi hiyo kana kwamba ni kazi ya kudhalilisha mno; hawatambui kwamba
kuna mbaraka ndani yake kwa ajili yao wenyewe na familia zao. Yale yote wanayofahamu wao ni
kwamba kazi hiyo ni utumwa wa aina fulani. Mashamba yao ya miti izaayo matunda huachwa bila
kutunzwa, mazao hayapandwi kwa majira yake yanayofaa, na kazi ya juu juu tu hufanywa katika
kuilima ardhi hiyo. ----- Fundamentals of Christian Education, uk. 326,327. (1894)
Matunda, Mboga za Majani, na Kuku Vyapendekezwa kwa Eneo Moja
Katika ujirani huu kuna eneo kubwa la ardhi isiyokaliwa na watu. Baadhi ya watu wetu wanaoishi
katika mazingira ya hali ya hewa iliyosumishwa huko mijini wangeweza kunufaika kwa kujipatia
ekari chache za ardhi hii. Wangeweza kujipatia mahitaji yao ya maisha kwa kupanda matunda na
mboga za majani na kufuga kuku. Hospitali yetu ingefurahi kununua mayai na mboga za majani
kutoka kwao. Natamani kwamba m radi fulani kama huo ungeanzishwa hapa. Baraka kubwa
ingewajia wazazi hao pamoja na watoto wao, endapo wangeondoka katika miji hiyo miovu,
iliyochafuliwa na kwenda katika sehemu zile za shamba [vijijini]. ----- Letter 63, 1904.
Kuishi Mashambani [Vijiji ni] - Mbaraka Kwa Maskini
Endapomaskini ambao hivi sasa wamesongamana mijini wangepata makazi yao huko
mashambani [vijijini], wasingeweza kujipatia riziki yao tu, bali wangepata afya na furaha ambayo
mpaka sasa hawaijui. Mara nyingi [huko mijini] kazingumu, chakula duni, na kubana mno
matumizi, shida na umaskini, hiyo ndiyo ingekuwa sehemu ya maisha yao. Lakini ni mbaraka
ulioje ambao ungekuwa wao kama wangeondoka mjini, na kuviachilia mbali vishawishi vyake
vinavyowaelekeza watu maovuni, kuachana na machafuko yake na uhalifu, huzuni na uchafu wake,
na kwenda mashambani [vijijini] kwenye utulivu na amani na usafi.
Kwawengi miongoni mwa wale wanaoishi mijini ambao hawana hata kipande kidogo cha majani
mabichi cha kuweza kuweka miguu yao juu yake, ambao mwaka nenda mwaka rudi wameziangalia
nyua zao zilizojaa uchafu na njia zile finyu za vichochoroni, kuta zile za matofali ya kuchoma na
sakafu za mawe za kutembea juu yake, mbingu zile zilizojaa vumbi na moshi, ----- kama hao
wangepelekwa kwenye wilaya m oja yenye mashamba ya kulima, yaliyozungukwa na mashamba ya
chanikiwiti, misitu midogo, na vilima na vijito, mbingu safi na zenye hewa safi, na hewa safi ile ya
mashambani, basi, kwao hao ingekuwa karibu sawa na [kuishi] mbinguni.
Mawasilianoyao yakiwa yamekatwa kwa kiwango kikubwa hata wasiweze kuonana na watu
wengine wala kuwategemea, tena wakiwa wametengwa mbali na semi zile chafu za ulimwengu
pamoja na desturi zake na misisimko yake, wangeweza kukaribia sana kwenye maana ya ndani
kabisa ya maumbile. Kuwako kwake Mungu kungesikika na kuwa dhahiri sana kwao. Wengi
wangejifunza kwake fundisho lile la kumtegemea yeye. Kupitia katika maumbile hayo wangeweza
kuisikia sauti yake mioyoni mwao ikiwatamkia amani na upendo wake, na akili na roho na mwili
wao vingeweza kuitikia uponyaji huo, ulio na uwezo wa kuwapa uzima. ----- The Ministry of
Healing, uk. 190- 192. (1905).
Viwanda Vidogo Mbalimbali Kwa Familia Zitokazo Mijini
Wauminiwale ambao kwa sasa wanaishi mijini inawapasa kwenda shamba [vijijini], ili wapate
kuwaokoa watoto wao na maangamizi. Mawazo yanapaswa kuelekezwa upande wa kuanzisha
viwanda [vidogo] ambamo familia hizo zinaweza kupata kazi. Wale wanaosimamia kazi ya Shule
na wangeona kile kinachoweza kufanywa na taasisi hizo zingeweza kuanzishaviwanda [vidogo]
kama hivyo, ili watu wetu wanaotaka kuondoka mijini, waweze kujipatia makazi yao yanayofaa
bila kutumia fedha nyingi sana, na pia kuweza kupata kazi huko. Katika sehemu zote mbili na kuna
hali nzuri ya ardhi ambayo inatia moyo kuweza kuuendeleza mpango kama huo. Jifunzeni hali ya
nchi ilivyo.
Yaleyote yanayotakiwa kufanywa hayawezi kuelezwa kinagaubaga mpaka hapo mwanzo
utakapofanywa. Liombeeni jambo hilo, tena kumbukeni kwamba Mungu ameshika usukani,
kwamba yeye ndiye anayeongoza katika shughuli zote za kibiashara. Mahali pale kazi
inapoendeshwa kwa njia inayotakiwa panakuwa fundisho la mfano linalopaswa kuigwa na mahali
pengine [patakapofunguliwa]. Pasiwe na ufinyu wo wote [wa mawazo], wala ubinafsi, katika kazi
hiyo inayofanyika mahal i hapo. Kazi hiyo inatakiwa kuwekwa juu ya msingi rahisi, unaoweza
kutekelezwa. Wote hawana budi kufundishwa ya kuwa sio tu kukiri kwamba wanaiamini kweli,
kama vile kweli yenyewe ilivyo, bali kuionyesha kweli hiyo kwa mfano katika maisha yao ya kila
siku. ----- Letter 25, 1902.
Kazi ya Kuuza Chakula Kiletacho Afya
Shughuli [biashara] hiyo ya [kuuza] chakula kiletacho afya inapaswa kuanzishwa hapa
[Avondale]. Hiyo ingekuwa mojawapo ya viwanda vinavyohusiana na Shule. Mungu ameniagiza
mimi kwamba wazazi wanaweza kupata kazi katika kiwanda hicho, na kuwapeleka watoto wao
shuleni. Lakini kila kitu kinachofanyika hapo kinapaswa kufanywa kwa njia iliyo rahisi sana.
Pasiwepo na ubadhirifu [matumizi mabaya] wo wote katika jambo lo lote lile. Kazi thabiti
inapaswa kufanywa, kwa sababu kazi isipofanywa kwa uthabiti, matokeo yake yatakuwa kazi ya
ovyo ovyo tu. ----- Australasian Union Conference Record, Julai 28, 1899.
SEHEMU YA TANO
Kujiandaa kwa Hatari Kubwa Itakayoletwa na Amri ya Jumapili
Nyakati za Taabu Ziko Mbele Yetu
Haitupasisisi kujiweka wenyewe mahali ambapo tutalazimishwa kuwa na uhusiano wa karibu
sana na wale wasiomheshimu Mungu.... Hatari kubwa karibu sana inakuja kuhusiana na utunzaji
wa Jumapili....
Kundi la Jumapili linajiimarisha lenyewe katika madai yake ya uongo, na jambo hilo litamaanisha
mateso kwa wale wanaokata shauri kuitunza Sabato ya Bwana [Jumamosi]. Yatupasa kujiweka
wenyewe mahali pale tutakapoweza kuishika amri hiyo ya Sabato [Jumamosi] kwa u kamilifu wake.
"Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu
wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote." Tena yatupasa kuwa waangalifu tusijiweke mahali pale
itakapokuwa vigumu kwetu sisi wenyewe na watoto wetu ku itunza Sabato [Jumamosi].
Endapokwa maongozi yake Mungu tunaweza kujipatia mahali pa kuishi mbali na miji, basi,
Bwana angependa kwamba sisi tufanye hivyo. Nyakati za taabu ziko mbele yetu. ----- Manuscript
99, 1908.
Harakisheni Kujiweka Tayari
Uwezo waliopewa wafalme [Ma- Rais] ukifungamana na wema ni kwa sababu yule aliyeshika
madaraka hayo yuko chini ya uongozi wa Mungu. Uwezo huo unapofungamana na uovu, basi,
unafungamana na nguvu za Shetani, nao utafanya kazi ya kuwaangamiza wale walio mali yake
Bwana. Ulimwengu wa Kiprotestanti umeisimamisha sanamu ya sabato [Jumapili] mahali pale
ambapo Sabato ya Mungu [Jumamosi] ingepaswa kusimama, nao wanatembea katika nyayo za
Upapa. Kwa sababu hiyo mimi nauona umuhimu kwa watu wa Mungu kuondoka mijini kwenda
kwenye sehemu za upweke huko mashambani [vijijini], ambako wanaweza kulima mashamba yao
na kuzalisha wenyewe mazao yao. Kwa njia hiyo wanaweza kuwalea watoto wao kuwa na tabia ya
kawaida, inayoleta afya. Nauona umuhimu wa kuharakisha kuyaweka mambo yote tayari ili
kuweza kukabiliana na hatari hiyo kubwa. ----- Letter 90, 1897.
SURA YA SITA
Tusikae Wengi Mahali Pamoja Katika Vituo Vya Taasisi Zetu
Tusikae Wengi Mahali Pamoja
Katika siku zetu hizi Bwana anataka watu wakewatawanyike ulimwenguni kote. Haiwapasi kukaa
wengi mahali pamoja. Yesu alisema, "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila
kiumbe [mtu]." Marko 16:15. Wanafunzi walipofuata mapenzi [matakwa] yao ya kubaki kwa idadi
kubwa kule Yerusalemu, mateso yaliruhusiwa kuwapata, nao wakatawanyika kwenda mahali pote
katika ulimwengu ule uliokaliwa na watu.
Kwamiaka mingi ujumbe huu wa onyo na wa kuwasihi umekuwa ukija kwa watu wetu,
ukiwashurutisha kusonga mbele na kuingia katika shamba la Bwana la mav uno, na kufanya kazi
bila kujifikiria wenyewe kwa ajili ya roho za watu. ----- Testimonies, Gombo la 8, uk 215. (1904)
Tawanyikeni Na Kwenda Kule Wasikolipata Onyo Hilo
Washirikiwa makanisa yetu makubwa ni wengi ambao karibu hawafanyi kitu cho chote kabisa.
Hao wangeweza kufanikiwa kufanya kazi nzuri kama wangeweza kutawanyika na kwenda mahali
ambako kweli hii bado haijaingia badala ya kujikusanya wengi mahali pamoja. Miti iliyopandwa
karibu karibu sana haisitawi. Hupandikizwa mahali pengine na mwenye bustani ili ipate nafasi ya
kutosha kukua, isizuiwe kukua zaidi wala isiwe dhaifu. Kanuni iyo hiyo ingefanya kazi yake vizuri
kwa makanisa yetu makubwa. Wengi miongoni mwa washiriki wetu wanakufa kiroho kwa kukosa
kazi hii hii [ya kwenda mahali kule am bako ujumbe bado haujafika]. Wanakuwa dhaifu, tena
wanashindwa kufanya kazi yao vizuri. Wangepandikizwa [wangehamia] mahali pengine,
wangeweza kupata nafasi ya kutosha kuweza kukua [kiroho] na kuwa na nguvu.
Si kusudi lake Mungu kwamba watu wake wakae wengi mahali pamoja, au waishi pamoja katika
jumuia kubwa. Wanafunzi wa Yesu ni wawakilishi wake hapa duniani, na Mungu anakusudia
kwamba wao watatawanyika kila mahali duniani, katika miji midogo, miji mikubwa, na vijijini, na
kuwa kama mianga kati ya giza n ene la ulimwengu huu. Wanapaswa kuwa wamishonari wa
Mungu, kwa imani yao wakishuhudia ukaribu sana wa marejeo ya Mwokozi wao.
MAHALI PALE ILIPOFUNGUKA NJIA YA KUJIPATIA RIZIKI
Washirikiwalei [wa kawaida] wa makanisa yetu wanaweza kufanikiwa kufanyakazi ile ambayo,
hata sasa, hawajaanza kuifanya. Wasiwepo watu wanaohamia mahali papya kwa ajili ya faida ya
kidunia tu; bali mahali pale ilipofunguka njia ya kujipatia riziki ziende familia zile zilizojizatiti
katika kweli, familia moja au mbili hivi ziende mahali pamoja kufanya kazi kama wamishonari.
Wangejisikia kuwa wanayo haja ya kuwapenda watu, kwamba wanao mzigo wa kuwashughulikia
watu hao, tena, kama somo lao, wangejifunza namna ya kuwaingiza katika kweli hii. Wanaweza
kugawa vitabu vyetu, kufanya mikutano nyumbani mwao, kufahamiana na majirani zao, na
kuwaalika waje kwenye mikutano hiyo. Wanaweza kuiacha nuru yao kuangaza kwa matendo yao
mema. ----- Testimonies, Gombo la 8, uk. 244,245. (1904)
Vishawishi Vya Taasisi Zetu Visiwavute
Walewanaojisikia kupenda kuishi karibu na nyumba yetu ya kuchapisha vitabu au hospitali na
shule yetu iliyo kwenye bustani ile kubwa ya Takoma [Takoma Park] hawana budi kupata ushauri
kabla hawajahamia huko.
Kwa wale wanaotarajia kwenda kule Mountain View kama n dipo mahali pazuri pa kuishi, ati kwa
sababu tu mtambo wetu wa kuchapisha vitabu wa Pasifiki [Pacific Press] utajengwa pale,
ningependa kuwaasa hivi: Zitupieni macho sehemu nyingine za ulimwengu zinazohitaji nuru yenu
mliyoipokea kama amana. Kumbukeni kwam ba Mungu amempa kila mtu kazi yake. Chagueni
mahali fulani mtakapokuwa na nafasi nzuri ya kuiacha nuru yenu kuangaza kati ya giza hilo la
kimaadili.
Inatokeasikuzote ya kwamba taasisi yetu inapojengwa mahali fulani, ziko familia nyingi
zinazotaka kwendahuko na kuweka makao yao karibu nayo. Hivyo ndivyo ilivyokwisha kutokea
kule Battle Creek na Oakland, na, kwa kiwango fulani, karibu kila mahali ambapo tunayo shule au
hospitali yetu. ----- Fundamentals of Christian Education, uk. 494,495. (1904).
Msianzishe Vituo Vya Yerusalemu
Watuwetu ... hawapaswi kupaangalia ... kama kituo cha Yerusalemu. Wasifikiri kwamba kwa
sababu idadi fulani ya ndugu zetu wameitwa kuja hapa kujiunga na kazi hii ya uchapishaji, basi,
hapa ndipo mahali pa kukaa idadi kubwa ya watu wetu na familia zao. Na kila mtu anayehusika na
Ofisi hiyo ajiweke tayari kuondoka endapo Mungu atamwita kwenda mahali fulani papya. -----Manuscript 148, 1905.
Msisongamanemahali pamoja, mkifanya kosa lile lile lililokwisha kufanywa kule BattleCreek.
Kuna mamia ya mahali pengine panapohitaji nuru hiyo aliyowapa Mungu. ----- Fundamentals of
Christian Education, uk. 495. (1904).
Bakini Katika Makanisa Madogo - Anzisheni Shule Nyingi Mpya
Familia nyingi ambazo, kwa madhumuni ya kuwapatia el imu watoto wao, huhamia mahali kule
zilikojengwa shule zetu kubwa, wangeweza kufanya kazi bora kwa ajili ya Bwana kwa kuendelea
kubaki pale pale walipo. Wangelitia moyo kanisa ambalo wao ndio washiriki wake kujenga shule
ya kanisa ambayo watoto walio katika mipaka yake wangeweza kujipatia elimu kamili ya Kikristo
itakayowawezesha kufanya kazi yao. Lingekuwa ni jambo bora sana kwa watoto wao, kwao
wenyewe, na kwa kazi ya Mungu, kama wangeendelea kubaki katika makanisa hayo madogo,
ambamo msaada wao unahitaji ka badala ya kwenda kule yaliko makanisa yetu makubwa, ambako,
kwa vile wao hawahitajiki [hawatakuwa na kazi kanisani], kuna majaribu daima ya kuanguka
katika uzembe [uvivu] wa kiroho.
Po pote pale walipo Wasabato wachache, wazazi wangeungana pamoja na k utenga eneo kwa ajili
ya shule ya kutwa ambamo watoto na vijana wao wanaweza kupata mafunzo yao. Wamwajiri
mwalimu Mkristo, ambaye, kama mmishonari aliyejitoa wakf, ataweza kuwaelimisha watoto wao
kwa njia ambayo itawafanya nao wawe wamishionari. ----- Counsels to Teachers, uk. 173,174.
(1913)
Hivi Malaika Wanajisikiaje
Nafikiriajinsi malaika wanavyojisikia wanapouona mwisho ule ukikaribia, na kuwaona wale
wanaodai kuwa wanayo maarifa ya kumjua Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma, wakisongamana
sana mah ali pamoja, wakikaa wengi mahali pamoja, na kuhudhuria mikutano yao, na kuwa na hisia
ya kukata tamaa na kutoridhika endapo hakuna mahubiri mengi yanayozinufaisha roho zao na
kuliimarisha kanisa, wakati wao hawafanyi kazi yo yote kabisa. ----- Letter 16e, 1892.
Ipanueni Kazi na Kuieneza - Ila Sio Pale Makao Makuu
Watuwanahamasishwa [wanatiwa moyo] kulundikana pale Battle Creek, tena wanalipa zaka yao
na kutoa mvuto wao ili ipate kujengwa Yerusalemu ya leo pale ambayo haifuati mpango wa
Mungu. Kwa ku fanya kazi hiyo mahali pengine panakosa msaada ambao wangeweza kuupata.
Panueni kazi, enezeni, naam; lakini sio mahali pamoja. Tokeni na kujenga vituo vyenye mvuto
mahali pale ambapo hakuna kitu au karibu hakuna cho chote kilichofanyika pale. Livunje- vunje ni
kundi hilo kubwa sana lililosongamana mahali pamoja; tawanyeni miali ya nuru ile iokoayo, na
kuiangaza nuru hiyo katika pembe [kona] za dunia zilizotiwa giza. ----- Testimonies to Ministers,
Uk. 254,255. (1895)
SEHEMU YA SABA
Kuongozwa na Maongozi ya Mungu
Mungu Anapoifungua Njia
Wakatiumefika, ambapo, kadiri Mungu anavyoifungua njia, familia hazina budi kutoka mijini.
Watoto wapelekwe kule shamba [vijijini]. Wazazi na wajipatie mahali panapofaa kulingana na
fedha walizo nazo zitakavyoruhusu. Ingawa nyumba ile iliyojengwa inaweza kuwa ndogo, hata
hivyo, pangekuwapo na shamba linaloweza kulimwa kuambatana nayo. ----- Manuscript 50, 1903.
Mungu Atawasaidia Watu Wake
Wazaziwanaweza kujijengea nyumba ndogo huko shamba [vijijini], na kuwa na mashamba ya
kulima, ambamo wanaweza kuwa na viunga vya miti ya matunda, na kupanda mboga za majani
pamoja na matunda madogodogo ili kuchukua mahali pa nyama, ambayo inaichafua sana damu
inayopita katika mishipa na kuleta uzima. Mahali hapo watoto hawatazungukwa na mivuto ile
miovu ipatikanayo katika maisha yale ya mjini. Mungu atawasaidia watu wake kupata makazi
kama hayo nje ya miji [wakimwomba]. ----- Medical Ministry, uk. 310. (1902)
Kusaidia Kuifungua Nj ia
Wakatiunapozidi kusonga mbele, watu wetu wengi zaidi na zaidi watalazimika kuihama miji.
Kwa miaka mingi tumeagizwa ya kwamba ndugu na dada zetu, na hasa familia zile zenye watoto,
wangefanya mpango wa kuondoka mijini kwa kadiri njia inavyofunguka mbele yao na
kuwawezesha kufanya hivyo. Wengi watalazimika kufanya kazi ngumu kwa bidii ili kusaidia
kuifungua njia. Lakini mpaka hapo itakapowezekana kwao kuhama, kadiri wanavyoendelea kubaki
humo, wangefanya bidii kubwa sana kufanya kazi ya umishonari, h aidhuru eneo la mvuto wao liwe
dogo jinsi gani. ----- Review and Herald, Sept. 27, 1906.
Ushauri na Onyo Kwa Wale Wanaotarajia Kuondoka Mijini
[Baruahii iliandikwa Desemba 22, 1893, kuijibu barua iliyotoka kwa kiongozi maarufu wa Battle
Creek, akimjulisha Bibi White kuwa kama itikio lao kwa onyo lile linalowataka watu wetu kuhama
kutoka Battle Creek, "kati ya watu mia moja na mia mbili" hivi walikuwa wanajiandaa kuondoka
"kwa haraka iwezekanavyo." ----- WAKUSANYAJI WA MAANDIKO.]
Nduguyangu, baruayako inaniambia kwamba wapo wengi waliopata mwamko mkubwa wa
kuondoka Battle Creek. Ipo haja, haja kubwa, ya kazi hiyo kufanyika, na kufanyika sasa. Wale
wanaojisikia kuhama hivi mwishoni hebu isiwe kwa kukurupuka, kwa msisimko, au bila kufikiri,
au kwa n jia ambayo hatimaye watajuta sana kuhama kwao....
Angalienisana pasiwepo na kuhama kunakofanywa bila kufikiri katika kulitii onyo hilo la kuhama
kutoka Battle Creek. Msifanye jambo lo lote bila kuitafuta hekima toka kwa Mungu, ambaye
ameahidi kuwapa kwaukarimu wale wote wamwombao, na ambaye hakemei [Yakobo 1:5]. Yale
yote ambayo mtu ye yote anaweza kufanya ni kuwapasha habari tu na kutoa ushauri wake, kisha
kuwaacha wale wanaoamini kwa dhati kuhusu wajibu wao wa kuhama, wakiwa chini ya uongozi
wake Mungu, kufanya hivyo; mioyo yao yote ikiwa imefunguliwa wazi ili wapate kujifunza na
kumtii Mungu.
Miminasumbuka sana moyoni mwangu kufikiri kwamba huenda wapo hata baadhi ya waalimu
[wachungaji, n.k.] wetu ambao wanahitaji kuwa na busara zaidi ili waweze k ufikiria pande zote [za
jambo hilo]. Wajumbe wale wanaouchukua ujumbe huo wa rehema kwa ulimwengu wetu, ambao
wanategemewa na watu wetu, wataombwa kutoa mawaidha [maoni] yao. Tahadhari kubwa haina
budi kutumika kwa upande wa watu hao ambao hawana uzoefu halisi wa maisha ya kujitegemea
[vijijini] kwa kufanya kazi [kwa mikono yao], na ambao watakuwa hatarini kutoa mawaidha yao,
wasijue mawaidha yao hayo yatasababisha watu wengine kufanya kitu gani.
KIPAWA CHA KUTOA USHAURI
Watuwengine wanaona mbali katika mambo mengi, hao wanao uwezo wa kutoa ushauri. Ni
kipawa cha Mungu. Katika nyakati zile ambazo kazi ya Mungu inahitaji maneno ya busara na ya
dhati, na yale yaliyo thabiti, hao wanaweza kusema maneno fulani ambayo yatawafanya watu wale
waliochanganyikiwa pamoja na wale walio gizani [wasioelewa kitu], kuiona kwa ghafula, kama
vile nuru ya mwanga wa jua inavyomulika ghafula, njia ile wanayopaswa kuifuata katika jambo lile
lililowajaza mashaka mengi na kuifadhaisha sana mioyo yao wakati walipokuwa wakifan ya
uchunguzi wao uliowachukua majuma mengi na miezi mingi. Ufumbuzi upo, yaani, ufyekaji wa
njia ile iliyo mbele yao, na Mungu ameruhusu mwanga wake wa jua kuingia mawazoni mwao, nao
wanaona ya kuwa maombi yao yamejibiwa, yaani, njia yao iko wazi. Lakini basi, mawaidha fulani
yanaweza kutolewa bila kufikiri, yakisema ----- tokeni tu Battle Creek, wakati hakuna maelezo yo
yote yaliyofafanuliwa vizuri kuhusu maendeleo gani watakayofanya katika maisha yao ya kiroho
kwa ajili yao wenyewe au kwa ajili ya wenginekwa kuichukua hatua hiyo [ya kuhama].
FIKIRIENI KWA MAKINI SANA KILA HATUA YA KUHAMA KWENU
Hebu kila mmoja awe na muda wa kutosha wa kufikiria [jambo hilo] kwa makini [uangalifu] sana;
asije akafanana na mtu yule aliyetajwa katika mfano [wa Yesu] aliyeanza kujenga, kisha
akashindwa kumaliza. Kuhama ko kote kusifanyike isipokuwa kama kuhama huko na matokeo
yake yote yamefikiriwa kwa makini sana ----- yaani, kila jambo limepimwa kuona uzito wake...
Kwa kila mtu kazi ilitolewa kulingana na uwezo wake.Basi, asihame akiwa na mashaka, bali
ajizatiti, na wakati uo huo akiwa ananyenyekea kwa kumtegemea Mungu.
Huendawakawapo watu ambao watataka kuharakisha kufanya jambo fulani, na kujiingiza katika
shughuli fulani ambayo hawaijui kabisa. Mambo hayo Mungu hataki. Fikiri kwa moyo mnyofu,
kwa maombi, ukijifunza Neno [la Mungu] kwa makini sana na kwa maombi, akili yako na moyo
wako vikiwa tayari kuisikiliza sauti ya Mungu.... Kuyajua mapenzi ya Mungu [katika suala hili] ni
jambo kubwa.
MIPANGO ILIYOPANGWA VIZURI INATAKIWA
Nayatoamaneno haya kwa kanisa lile lililoko kule Battle Creek ili lipate kutembea katika
mashauri ya Mungu. Haja ipo ya kuhama kwenu ----- yaani, wengi wenu kuhama kutoka Battle
Creek ----- tena, ipo haja pia ya ninyi kuwa na mipang o iliyopangwa vizuri juu ya kile
mtakachofanya mtakapohama toka Battle Creek. Msiende kwa kukimbia, bila kujua
mnachofanya.... Laiti kama wangekuwapo majenerali wenye hekima, wanaowafikiria wengine,
watu wale wanaoyachunguza mambo kwa kuangalia kila upande, watakaokuwa washauri salama,
ambao kidogo wanajua kile kilichomo ndani ya mwanadamu, wale ambao wanajua kuongoza na
kushauri katika kicho chake Bwana.
HATARI INAAMBATANA NA UZOEFU MPYA
Nimekwishakuona kwamba hatari inaambatana na kila awamu mpya ya uzoefu kanisani, kwa
sababu wengine wanayasikia mambo hayo kwa moyo wenye kusisimka sana. Wakati waalimu
[wachungaji, n.k.] wengine wanaweza kuwa imara upande ule wa kufundisha mafundisho ya
Biblia, si wote watakaokuwa wamepata uzoefu wa maisha ya kujitegemea, si wote
watakaowashauri wale waliochanganyikiwa kwa hakika na usalama. Hawaitambui hali hiyo ya
kutatanisha ambayo haina budi kuja kwa kila familia itakayofanya mabadiliko hayo. Kwa hiyo,
wote wawe waangalifu sana kuchunga maneno yao wanayosema; kama hawayajui mawazo ya
Mungu katika baadhi ya mambo, basi, wasiseme kabisa kwa kukisia- kisia tu au kwa kudhani kuwa
mambo hayo yako hivyo. Kama hawajui kitu cho chote kilicho dhahiri, hebu na waseme hivyo, na
kuwaacha watu kila mmoja peke yake wapate kumtegemea Mungu. Hebu maombi mengi
yafanyike, hata kwa kufunga, ili mtu ye yote asije akahama akiwa gizani [hajui la kufanya], bali
ahame akiwa nuruni [anajua la kufanya] kama vile Mungu alivyo nuruni....
HAMENI KWA HADHARI
Hebupasiwepo na kitu cho chote kinachofanywa bila utaratibu, isije ikatokea hasara kubwa au
kupoteza mali kwa sababu ya hotuba motomoto zilizotolewa zenye kujaa misisimko ndani yake
ambazo zinaamsha shauku ambayo haimo katika mpangilio wa Mungu, hata ushindi ule uliokuwa
wa lazima ku patikana uweze kugeuka na kuwa kushindwa kunakotokana na kukosa utulivu wa
kusimamia mambo vizuri na kuyafikiria vizuri, na kujenga juu ya kanuni na makusudi yaliyo
imara. Hebu na pawepo na uongozi wa busara katika jambo hilo, na wote wapate kuhama chini y a
uongozi ule wenye hekima wa Mshauri yule asiyeonekana, ambaye ni Mungu. Mambo ya
kibinadamu yatajitahidi kutawala, na huenda pakawa na kazi iliyofanyika ambayo haina sahihi
[idhini] ya Mungu. Basi, namsihi kila mtu asiwaangalie washiriki hao wa kibinadam u kwa nia na
imani thabiti sana, bali amwangalie kwa bidii nyingi sana Mungu, mshauri mmoja aliye a hekima.
Wekeni njia zenu zote na mapenzi [nia] yenu ili yapatane na njia za Mungu na mapenzi yake....
MATOKEO YA HATUA ZA HARARA
Endapowengine watah ama kwa haraka na kukimbia toka Battle Creek, halafu wakajikuta
wameingia katika hali ya kukata tamaa, basi, watatoa shutuma zao, sio juu yao wenyewe, kwa
kuhama kwao bila kutumia busara, bali juu wa wengine, ambao watawalaumu kuwa walitia
shinikizo lao ju u yao [mpaka wakawa wamehama]. Kutibuliwa kwa mipango yao yote na
kushindwa kwao kutawafanya wawarudishie shutuma zote wale ambao wasingestahili kupewa sifa
mbaya kama hizo....
Sasa, hivi sasa, ndio wakati ambao hatari zile kubwa za siku za mwisho zinazidi kuongezeka sana
kutuzunguka pande zote, tunahitaji watu wenye hekima kuwa washauri wetu, sio watu wale
watakaoona kwamba ni wajibu wao kuwasisimua watu na kuleta machafuko, bali ni wale wawezao
kutoa mashauri yao ya busara na kuratibu na kupanga mipangoili kwamba kila msisimko
unaotokea upate kuleta mpangilio mzuri kutoka katika machafuko yaliyopo, na kuleta raha na
amani kwa njia ya kulitii Neno la Bwana. Hebu kila mtu na apatikane mahali pake panapomfaa
hasa, ili apate kumfanyia Mungu kazi fulani, kul ingana na uwezo wake aliopewa....
Kwajinsi gani jambo hilo litaweza kufanyika? "Jitieni nira yangu," asema Yesu Kristo, yule
aliyewanunua ninyi kwa damu yake ya thamani, ninyi ambao ni watumishi na mali yake, "mjifunze
kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi." Endapo kila mmoja atakuja kwa
Yesu akiwa na moyo ulio tayari kufundishwa, moyo wenye toba, hapo ndipo atakuwa katika hali ya
kiakili ya kuwezakufundishwa na kujifunza kwa Yesu na kuyatii maagizo yake....
WEKENI KILA MPANGO MLIO NAO MBELE ZAKE MUNGU
Hatuwezi kuwa na imani dhaifu sasa; hatuwezi kuwa salama kwa kuwa na mtazamo ulio mlegevu,
wa kivivu, na wa kizembe. Kila chembe ya nguvu yetu inapaswa kutumika, na fikira kali, tulivu,
zenye kina zinapaswa kutumika. Hekima ya mjumbe ye yote wa kibinadamu haitoshi katika
kupanga mipango na kubuni mbinu kwa wakati kama huu. Wekeni kila mpango mlio nao mbele
zake Mungu kwa kufunga pamoja na kujinyenyekeza nafsi zenu mbele zake Bwana Yesu, na
kuzikabidhi njia zenu kwa Bwana. Ahadi ya hakika ni hii, "Naye atayanyosha mapito yako
[Atakuongoza katika njia zako - Mithali 3:5,6]. Yeye hana kikomo katika uwezo wake wa kusaidia.
Mtakatifu wa Israeli, anay eliita jeshi lote la mbinguni kwa majina yake, na kuzishikilia nyota za
mbinguni mahali pake, anawatunza ninyi kila mmoja peke yake....
Ningependakwamba wote wapate kutambua uwezekano na mwelekeo uliopo kwa wale wote
wanaomfanya Kristo kuwa utoshelevu wao na tegemeo lao. Uhai ule uliofichwa pamoja na Kristo
katika Mungu daima unalo kimbilio; mtu huyo anaweza kusema, "Nayaweza mambo yote katika
yeye anitiaye nguvu."
Jambohili nawaachieni mikononi mwenu; kwa maana nimekuwa na wasiwasi na kusumbuka sana
kwa ajili ya hatari zile zinazowashambulia wote walioko huko Battle Creek, ili wasije wakahama
bila kuwa na tahadhari kubwa na [kwa kufanya hivyo] kumpa yule adui yetu faida kubwa. Jambo
hilo halipaswi kuwa hivyo, maana kama tukienda kwa unyenyekevu na Mungu wetu, basi,
tutakwenda salama. ----- Letter 45, 1893.
SURA YA NANE
Vituo Vyetu vya Taasisi Kuwa Mbali na Msongamano wa Watu
Mahali Panapofaa Kujenga Taasisi Zetu
Agizo[lile lile] bado linazidi kutolewa, Tokeni mijini. Jengeni hos pitali zenu, shule zenu, na ofisi
zenu mbali na vituo vyenye watu wengi. Wengi kwa wakati huu wanaomba sana ili wapate kubakia
mijini, lakini wakati utakuja, muda si mrefu kuanzia sasa, ambapo wale wote wanaotaka kuziepuka
tamasha na sauti hizo za uovu wat akapohama na kwenda shamba [vijijini]; kwa maana uovu na
uchafu utaongezeka kwa kiwango ambacho mazingira yote ya mjini yataonekana kana kwamba
yamechafuliwa. ----- Letter 26, 1907.
Kuepuka Majaribu na Ufisadi
Wenginewameshangaa kwa nini ofisi yetu ya uchapishaji inatakiwa kuhamishwa toka Oakland
kwenda Mountain View. Mungu amekuwa akiendelea kuwaita watu wake kuondoka mijini. Vijana
wetu ambao wamefungamana na taasisi zetu hawapaswi kuwekwa mahali pale watakapoweza
kukabiliwa na majaribu na ufisadi unaoonekana katika miji mikubwa. Mountain View
pameonekana kuwa ni mahali panapofaa kwa ofisi yetu ya uchapishaji. ----- Manuscript 148, 1905.
Nyakati za Dhoruba Zi Mbele Yetu
Jangahilo [la kuteketezwa kwa moto jengo la Review and Herald] linawezakuleta mabadiliko
dhahiri katika mambo yetu. Natumaini kwamba ndugu zetu hao watalizingatia fundisho hilo
ambalo Mungu anataka kuwafundisha, na ya kwamba hawatarudia kuijenga tena nyumba ya
uchapishaji pale Battle Creek. Mungu anamaanisha kwamba sisi hatu takaa mijini; maana zinakuja
nyakati za dhoruba kali sana mbele yetu. ----- Letter 2, 1903.
Mahali Wanapoweza Kufundishwa Kwa Ufanisi Vijana Wetu
Mungu ametuma kwetu onyo baada ya onyo ya kwamba shule zetu na nyumba zetu za uchapishaji
pamoja na hospitali zetu hazina budi kujengwa nje ya mji, mahali wanapoweza kufundishwa kwa
ufanisi vijana wetu kuhusu kweli ni nini. Asiwepo mtu ye yote anayezitumia Shuhuda [zangu]
kutetea ujenzi wa shughuli zetu kubwa za kibiashara mijini. Msiitangue nuru iliyokwish a kutolewa
kwetu juu ya somo hilo.
Watuwatainuka [watatokea] wakisema mapotovu, wakifanya kazi yao kupinga mambo yale yale
ambayo Bwana anawaongoza watumishi wake kufanya. Lakini wakati umewadia kwa wanaume na
wanawake kufikiri kwa kulinganisha chanzo cha jambo na matokeo yake. Tumechelewa mno,
tumechelewa mno kuanzisha mashirika makubwa ya biashara mijini ----- tumechelewa mno
kuwaita vijana wetu wa kiume na wa kike watoke vijijini kuja mjini. Hali zinaendelea kujitokeza
mijini zitakazofanya iwe vigumu sana kwa wale wa imani yetu kuendelea kubaki humo. Kwa hiyo,
lingekuwa kosa kubwa sana kuweka fedha zetu katika ujenzi wa shughuli za kibiashara mijini. -----Manuscript 76, 1905.
Kuishughulikia Miji Kutoka Katika Vituo Vya Mbali
Kwakadiri inavyowezekana, taasisi zetu zingejengwa mbali na miji. Hatuna budi kuwa na
watenda kazi kwa taasisi hizo, na iwapo zinajengwa mjini, hiyo humaanisha kwamba watu wetu
hawana budi kukaa karibu nazo. Lakini si mapenzi ya Mungu kwamba watu wake wakae mijini
ambamo mn a ghasia nyingi [makelele] na machafuko. Watoto wao na waepushwe na hali hiyo;
maana mfumo mzima wa mwili huathirika kitabia kwa ghasia za kwenda huku na huko, kukimbiakimbia ovyo na makelele. Bwana anawataka watu wake wahamie kule shamba [vijijini], ambako
watakaa kwenye mashamba yao, na kupanda matunda yao pamoja na mboga za majani, tena,
mahali pale watoto wao wanapoweza kuangalia moja kwa moja kazi za Mungu katika maumbile
[viumbe vya asili]. Nendeni na familia zenu mbali na miji ndio ujumbe wangu.
Kweli ni lazima isemwe, haidhuru kama watu wataisikia [wataizingatia], au wataikataa. Miji
imejaa majaribu mengi. Tungepanga mipango yetu ya kazi, kwa kadiri iwezekanavyo, kwa namna
ambayo tutaweza kuwazuia vijana wetu wakubwa mbali na uchafu huo.
Mijii natakiwa kushughulikiwa kutokea kwenye vituo vya mbali. Akasema yule mjumbe wa
Mungu, "Je! hivi miji hiyo haitapewa onyo? Naam; si kwa njia ya watu wa Mungu kuishi humo,
bali kwa njia ya wao kuitembelea, na kuwaonya juu ya kile kinachokuja juu ya ulimwenguhuu." ----- Letter 182, 1902.
Mahali Pale Ambapo Ni Rahisi Kuifikia Miji Hiyo
Hebuwatu wenye akili timamu wachaguliwe, sio kwa kusudi la kutangaza kile wanachokusudia
kufanya, bali kwa ajili ya kutafuta mali ya kumiliki katika maeneo yale yaliyo katika wilaya za
vijijini, mahali pale ambapo ni rahisi kuifikia miji hiyo, panapofaa kujenga shule yetu ya mafunzo
kwa ajili ya watenda kazi wetu, mahali ambapo panaweza kujengwa huduma za kuwatibu watu na
kuwahudumia wale wasioijua kweli. Tafuteni mahali kama hapo nje tu ya miji mikubwa, mahali
ambapo majengo yanayofaa yanaweza kupatikana, aidha kama zawadi toka kwa wenye majengo
hayo, au kwa kuyanunua kwa bei nzuri kutokana na misaada ya fedha iliyotolewa kwa hiari toka
kwa watu wetu. Msijenge majengo katika miji hiyo iliyojaa makelele mengi. ----- Medical
Ministry, uk. 308,309. (1909).
Mafundisho Toka Kwa Henoko na Lutu
Sisikama watu wake Mungu wanaozishika amri zake [kumi] ni lazima kuihama miji. Kama vile
alivyofanya Henoko, hatuna budi kufanya kazi yetu [ya kuongoa roho] mijini, lakini tusikae humo.
----- Evangelism, uk. 78,79. (1899)
Maovuyanapozidi sana katika taifa lo lote lile, daima husikika sauti fulani inayotoa onyo na
mafundisho, kama vile sauti ya Lutu ilivyosikika kule Sodoma. Hatahivyo, Lutu angeweza
kuiokoa familia yake kutokana na maovu yale mengi, kama asingalikuwa amefanya makazi yake
katika mji ule mwovu, ambao ulikuwa umejaa uchafu mwingi. Mambo yote ambayo Lutu na
familia yake walifanya mle Sodoma wangeweza kuyafanya hata kama wangeishi mahali fulani
mbali kidogo na mji ule. Henoko alitembea na Mungu, lakini hakukaa katikati ya mji wo wote
uliochafuka kutokana na kila namna ya vitendo vya kikatili vya kutumia nguvu pamoja na uovu,
kama Lutu alivyofanya kule Sodoma. ----- Evangelism, uk. 79. (1903)
Makanisa, Ila Sio Taasisi, Kuwamo Mijini
Tenana tena Bwana ametuagiza sisi kuwa inatupasa kuishughulikia miji kutokea kwenye vituo
vyetu vilivyo mbali. Katika miji hiyo hatuna budi kuwa na nyumba zetu za ibada [makanisa], kama
kumbukumbu za Bwana, lakini taasisi za kuchapisha vitabu vyetu, za kuponya wagonjwa, na zile
za kuwafundisha watenda kazi wetu; zinapaswa kujengwa nje ya miji. Hasa ni muhimu kwamba
vijana wetu waepushwe na majaribu ya maisha ya mjini.
Inapatanana ag izo hilo, kwamba nyumba za kukutania [makanisa] zimenunuliwa na kuwekwa
wakf katika mji wa Washington na Nashville, ambapo nyumba za uchapishaji na hospitali zilizo
katika vituo hivyo zimejengwa mbali na sehemu za katikati za miji hiyo yenye msongamano wa
watu wengi sana, kama vituo vya kazi vilivyo mbali na mji. Huo ndio mpango uliofuatwa katika
kuziondoa nyumba nyingine za uchapishaji pamoja na hospitali na kuzijenga mashambani [vijijini],
na jambo hilo linafuatwa kule Uingereza kwa habari ya nyumba ya uchapishaji ya London pamoja
na shule ya mafunzo iliyopo pale. Hivi sasa tumepewa nafasi ya kusonga mbele kwa maongozi ya
Mungu yaliyofunuliwa kwa njia ya kuwasaidia ndugu zetu katika vituo hivyo muhimu na
vinginevyo kwa kuanzisha kazi yetu juu ya msingi uli o imara, ili ipate kuendelezwa mbele kwa
uthabiti. ----- Special Testimonies, Series B, No. 8, uk. 7,8. (1907)
Tunatakiwa kuwa na busara kama nyoka na wapole kama hua katika juhudi zetu za kutafuta mali
ya kumiliki kule shamba [vijijini] kwa bei ya chini , na kutoka kwenye vituo hivyo vya mbali
tunapaswa kuihudumia miji hiyo. ----- Special Testimonies, Series B, No. 14, uk. 7. (1902)
Ujumbe Tuliopewa na Bwana
"Tokeni mijini; tokeni mijini!" ----- huo ndio ujumbe alionipa Bwana. Matetemeko ya nchi
yanakuja; mafuriko yanakuja; sisi hatutakiwi kujijenga katika miji hiyo miovu, ambamo yule adui
[Shetani] anatumikiwa kwa kila njia, na ambamo Mungu mara nyingi anasahauliwa. Mungu
anataka tuwe na macho safi ya kiroho. Yatupasa kuwa wepesi kutambua hatari ku bwa ambayo
ingeweza kuambatana na ujenzi wa taasisi zetu katika miji hiyo miovu. Yatupasa kupanga mipango
yetu kwa busara ili kuionya miji hiyo, na wakati uo huo kuishi mahali pale tunapoweza kuwakinga
watoto wetu pamoja na sisi wenyewe dhidi ya mivuto ilemichafu inayoharibu tabia ambayo
imeenea sana mahali hapo. ----- Life Sketches, uk. 409, 410. (1906)
SEHEMU YA TISA
Kukimbia Wakati wa Hatari Mwishoni mwa Pambano Hilo
Ishara ya Kuanza Kukimbia
Huusasa sio wakati kwa watu wa Mu ngu kuendelea kuyakaza mapenzi yao au kujilimbikizia
hazina zao katika ulimwengu huu. Wakati hauko mbali, ambapo sisi, kama wanafunzi wale wa
mwanzo [wa Yesu], tutalazimika kutafuta kimbilio letu maporini na mahali pasipo na watu. Kama
vile kule kuzingirwa kwa Yerusalemu na majeshi ya Warumi ilivyokuwa ishara ya kukimbia kwa
Wakristo wale wa Yudea, hivyo ndivyo, kule kujitwalia madaraka kwa upande wa taifa letu [la
Marekani] kwa njia ya kutunga amri ile inayowalazimisha watu wote kuitunza sabato ya papa
[Ju mapili], kutakavyokuwa onyo kwetu sisi. Wakati huo ndipo saa itafika ya kuondoka katika miji
mikubwa, tukijiandaa kuihama miji midogo ili kwenda mafichoni kwenye makazi yale ya upweke
katika milima. Na, kwa sasa, badala ya kutafuta hapa [duniani] makazi yaliyojengwa kwa gharama
kubwa, tungekuwa tunajiandaa kuhamia kwenye nchi ile iliyo bora, yaani, ile ya mbinguni. Badala
ya kutumia fedha zetu kwa kujifurahisha nafsi zetu, tungekuwa tunajifunza kubana matumizi
[kutumia fedha zetu kwa uangalifu sana]. ----- Testimonies, Gombo la 5, uk. 464,465. (1885)
JIPATIE VITABU HIVI VIPYA KABISA!
Vitabuvipya kadhaa vimekwisha kuchapishwa na vingine vimo mbioni kuchapishwa. Wasomaji
wanaotaka kujua habari zaidi pamoja na bei za vitabu hivyo wanaombwa kuandika barua zao kwa
Leaves of Life International, P.O. Box 17, MAFINGA, Tanzania: -1. KRISTO NA HAKI YETU, na E. J. Waggoner.
Kitabu hiki ni muhimu kwa kila Mkristo anayetaka wokovu ili awe tayari kumlaki Yesu
hewani.
2. UPONYAJI WA MUNGU, na Mary Ann McNeilus, M.D.
Kitabu hiki ni muhimu kuwa nacho. Punguza gharama za matibabu kwa kutumia njia 8
rahisi ambazo hazigharimu fedha. Epukana na magonjwa yasiyokuwa ya lazima. Jifunze
matumizi ya maji na mkaa kwa tiba rahisi za kushangaza.
3. MWITO WETU MKUU, na E. G. White.
Kitabu cha kesha la asubuhi kwa mwaka mzima. Kila robo mwaka ina kijitabu chake.
Robo nne hufanya kitabu kizima cha kudumu. Usizitupe. Tunza kwa matumizi ya kila
mwaka.
4. MNYAMA, JOKA, NA MWANAMKE, na Joe Crews.
Unabii unaolinganisha Pembe Ndogo ya Danieli 7 na Mnyama kama Chui wa Ufunuo 13.
Ni nani huyo? Ana athari gani kwako na kwa ulimwengu mzima? Usikikose kujipatia
kitabu hicho.
5. TOKA SABATO KWENDA JUMAPILI, na Carlyle B. Haynes.
Kitabu ulichokuwa ukikihitaji ili kujibu hoja zako zote juu ya Sabato na Jumapili.
Mabadiliko ya kalenda, sabato za kivuli, na kadhalika. Utunzaji wa Jumapili
ulivyoanza pamoja na semi mbalimbali za Viongozi wa Kiprotestanti juu ya Sabato.
6. UGONJWA NA SABABU YAKE, na E. G. White.
Kwa nini wanadamu wamedhoofika na wanazidi kudhoofika hivyo? Kwa nini ni vibaya
sana kuoana watu waliopitana umri kwa miaka mingi sana? Kuna madhara gani? Kwa
nini madawa ya kisasa ambayo ni sumu sio suluhisho kwa tiba halisi ya mwili? Usikose
kujipatia kitabu hiki.
7. IMANI NA MATENDO, na E. G. White.
Wengi wamechanganyikiwa kuhusu fundisho hilo la imani na matendo. Na wengi
watapoteza wokovu wao kwa kutokuwa na hakika juu ya mambo hayo mawili.
8. SIKU YA BWANA, na R. J. Wieland.
Kuna utata mkubwa kuhusu Siku ya Bwana miongoni mwa Wakristo. Wengine
wanadhani ni Jumapili, na wengine wanadhani ni Jumamosi. Biblia yasemaje?
Mwandishi huyu amelifafanua suala hili kwa njia rahisi kabisa.
9. MSALABA NA KIVULI CHAKE, na Stephen N. Haskell.
Somo la Patakatifu limeelezwa kwa njia rahisi sana inayoeleweka kwa mtu wa kawaida.
Huduma ya hekalu la duniani ilikuwaje? Huduma ya hekalu la mbinguni ikoje? Wokovu
wako unaathiriwaje na huduma ile ya mbinguni? Yesu anafanya nini sasa mbinguni?
Maswali hayo yanajibiwa. Sabato 7 za kivuli zaWakolosai 2:16,17 zimefafanuliwa humo.
10. HATARI KUBWA MBELE YETU, na Robert W. Olsen.
Matukio ya kutisha ya siku za mwisho yameelezwa waziwazi humo. Usikose kukinunua.
VITABU ZAIDI VINAANDALIWA KWA AJILI YAKO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni