MWONGOZO WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
Mwongozo wa Kanisa la Waadventista wa Sabato
Mafungu yote yaliyonukuliwa kwa ruhusa kutoka katika Biblia ya Kiswahili Union Version 1952 (Ilisahihishwa 1989)
ISBN 978
Haki miliki © 2013
Haki zote zimeifadhiwa hakuna ruhusa ya kunukuu au kupiga picha bila ruhusa ya wachapaji Tanzania Adventist Press
Dibaji ya Toleo la Kiswahili la Mwongozo wa Kanisa (2013)
Mwongozo wa Kanisa ambao kwa muda mrefu umekuwa ukichapishwa kama ‘Kanuni za Kanisa’, ulikuwa haujafanyiwa marekebisho kwa muda mrefu na hasa kwa kuzingatia ukuaji wa lugha ya Kiswahili ongezeko kubwa la istilahi ambao zinafaa zaidi kutafsiri maneno ambayo hapo mwanzo ilikuwa vigumu kuyatafsiri. Lakini pia mwongozo wa Kanisa umekuwa ukifanyiwa marekebisho kadhaa wakati wa vikao vya Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato, lakini baadhi ya marekebisho hayo hayakuingizwa ipasavyo katika tafsiri ya Kiswahili. Kwa sababu hiyo, toleo hili la Mwongozo wa Kanisakwa lugha ya Kiswahili, limezingatia matumizi sahihi ya lugha na istilahi za Kiswahili na kuingiza marekebisho yote kama yalivyochapishwa katika toleo la Kiingereza la mwaka 2010. Kwa hiyo watumiaji wa mwongozohuu wataona kuwa maneno au istilahi zilizokuwa zimezoeleka zimeachwa kwa sababu zilizoelezwa hapo juu. Mifano michache ya mabadiliko hayo ni
kama ifuatavyo.
1. Kitabu hiki chenye maelekezo ya uendeshaji wa kanisa mahalia kimezoeleka kuitwa ‘Kanuni za Kanisa’, lakini kusema kweli hii si tafsiri sahihi ya ‘Church Manual’, ‘manual ni ‘mwongozo’na kwa hiyo tafsiri sahihi ya jina la kitabu hiki ni Mwongozo wa Kanisa. Kwa sababu ya mazoea ya muda
mrefu na ili watu wasidhani kuwa hiki ni kitabu tofauti, majina yote mawili yamewekwa katika katika jalada la mwongozo huu. Lakini kwa ndani maneno ‘kanuni za kanisa’ yameachwa kabisa na badala yake kila mahali maneno ‘mwongozo wa kanisa’ yametumika.
2. Maneno ‘misingi ya imani’ yameachwa kwa kuwa si tafsiri sahihi ya ‘fundamental beliefs’. Maneno ya Kiingereza yanamaanisha imani (beliefs) 28 za msingi na si misingi
10
(foundations) 28 ya imani. Msingi ni mmoja ambapo juu yake kuna imani 28, yaani mambo 28 ambayo Waadventista wa Sabato wanayaamini. Kwa hiyo, badala ya ,misingi ya imani’, maneno yaliyotumika ni ‘imani za msingi’.
3. Mkutano wa washiriki wote wa kanisa mahalia umekuwa ukiitwa halmashauri au mashauri ya kanisa. Kulingana na Kamusi ya Kiswahili Sanifu, ‘halmashauri’ ni ‘kikundi cha watu maalum walioteuliwa au kuchaguliwa kuelekeza jambo fulani; bodi.’ Kwa hiyo si sahihi kuuuita mkutano wa watu wote halmashauri. Kwa hiyo badala ya halmashauri au mashauri ya
kanisa, toleo hili linatumia Mkutano Mkuu wa Kanisa.
4. Personal ministries imekuwa ikitafsiriwa kama ‘huduma za washiriki’ lakini tafsiri sahihi ya neno personal ni ‘–a mtu binafsi’. Kwa hiyo idara ya ‘personal ministries’ katika toleo hili imeitwa idara ya ‘huduma binafsi.’
5. Neno discipline katika Kiingereza lina maana mbili lakini neno nidhamu katika Kiswahili lina maana moja tu ya ‘utaratibu mzuri wa kuendesha jambo, adabu, staha’, lakini discipline inapomaanisha hatua zinazochukuliwa dhidi ya mtu aliyekosa nidhamu, neno nidhamu haliwezi kutumika. Neno sahihi katika Kiswahili ni ‘marudi’. Kwa hiyo, ‘marudi’ mahali ambapo hatua za kurudi mtu zinazungumziwa. Hali kama hiyo inajitokeza pia kwenye neno divorce. Katika Kiingereza ‘divorce’ ina maana ya kuachana lakini pia ina maana ya hati inayotolewa kwa walioachana. Katika Kiswahii ‘talaka’ ni ile hati na tendo la kuachana haiitwi ‘talaka’, ni ‘kuachana’. Kwa hiyo mahali ambapo divorce ina maana ya kuachana, neno ‘kuachana’ limetumiwa.
Kuna mifano mingi ambayo haiwezi kuorodheshwa yote katika nafasi hii ndogo ya dibaji lakini mifano hii michache imetolewa kuonesha sababu ya mabadiliko ya istilahi na misemo yaliyo katika
toleo hili. Ili kuwasaidia watu kuelewa baadhi ya istilahi na maneno
magumu, toleo hili lina orodha ya istilahi maneno hayo pamoja na
ufafanuzi wake.
11
Mashemasi wa Kike
Kuwekewa Mikono (tazama uk. ) Ingawa kuna vifungu katika mwongozo huu
vinavyoelekeza kuwekewa mikono kwa mashemasi wa kike (tazama uk, ), Divisheni
ya Afrika Mashariki na Kati haijalipokea jambo hili na kwa sababu hiyo
katika divisheni yetu tutaendelea kuwekea mikono mashemasi wa kiume tu.
Mashemasi wa kike wataendelea kuhudumu kama walivyokuwa wanafanya siku
zote bila kuwekewa mikono.
12
Kwa nini Kuwe
na Mwongozo wa Kanisa?
Kwa nini Kanisa la
Waadventista wa Sabato lina Mwongozo wa Kanisa?
Mungu ni Mungu wa
utaratibu kama ilivyodhihirika katika kazi zake za uumbaji na ukombozi.
Vivyo hivyo, utaratibu ni sehemu nyeti ya Kanisa lake.
Utaratibu hufikiwa kwa njia ya kanuni
na taratibu zinazoliongoza Kanisa katika utendaji wake wa ndani na
pia katika kutimiza utume wake duniani. Ili liwe jumuiya yakikanisa yenye
mafanikio katika kumtumikia Bwana na wanadamu, kanisa linahitaji
utaratibu, kanuni na nidhamu. Maandiko yanasisitiza kwamba “… mambo yote
na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.” (1 Kor. 14:40).
Ellen G. White alitaja
mahitaji hayo mwaka 1875: “Kanisa la Kristo liko hatarini wakati wote.
Shetani anajaribu kuwaangamiza watu wa Mungu, kwa hiyo, mawazo ya mtu
mmoja, maoni ya mtu mmoja, hayawezi kuaminika vya kutosha. Kristo
anataka
wafuasi wake wakusanyike
kama kanisa, wakifuata taratibu, wakiwa na kanuni na nidhamu, na wote
wakiwajibika kwa mwingine, huku wakiwachukulia wengine kuwa bora
kuliko wao wenyewe.”—3T 445.Lakini viongozi wa Kanisa hawakutoa haraka
kitabu cha kanuni kwa ajili ya uendeshaji wa Kanisa, ingawa Konferensi
Kuu ilikuwa inakutana kila mwaka katika miaka ya awali ya Kanisa na
wajumbe walikuwa wanaamua juu ya masuala ya utaratibu na uhai wa kanisa.
Hatimaye, mwaka 1882, Konferensi Kuu iliamua kuandaa “maelekezo kwa
viongozi wa kanisa, ili yachapwe katika Review and Herald au kama kitini.”
-RH, Des. 26, 1882. Jambo hili lilionesha utambuzi uliokuwa unaongezeka
kwamba utaratibu
13
ulikuwa muhimu kama
tulikuwa tunataka uendeshaji ufanye kazi kwa ufanisi na kufanana kwa
utaratibu kulikuwa kunahitaji misingi hiyo elekezi iwe katika
maandishi. Hata hivyo, pendekezo la kuziweka ibara hizo katika mfumo
wa kudumu kama mwongzo wa kanisa lilipoletwa mbele ya Konferensi Kuu
ya mwaka 1883, wajumbe walilikataa wazo hilo. Walikuwa wanahofia kuwa
jambo hilo lingefanya kanisa kuwa na utaratibu na kuwaondolea wachungaji
uhuru wao binafsi wa kushughulikia masuala ya utaratibu kama
waonavyo. Lakini hofu hiyo—ambayo bila shaka ilikuwa inaakisi
upinzani uliokuwepo miaka ishirini kabla dhidi ya muundo wa aina yoyote—ilianza
kutoweka. Mikutano ya kila mwaka ya Konferensi Kuu iliendelea
kushughulikia masuala ya utaratibu.Ingawa kanisa lilikuwa limekataa rasmi
kuwa na mwongozo, mara kwa mara viongozi walikuwa wanazikusanya na
kuziweka katika mfumo wa kitabu au kijitabu, kanuni za uhai wa kanisa
zilizokuwa zimekubalika. Pengine kilichokuwa kinavutia zaidi ni kitabu cha
kurasa 184 kilichochapishwa mwaka 1907 na mwasisi wa kanisa J. N.
Loughborough, kiitwacho “The Church, Its Organization, Order and
Discipline,”kilichokuwa kinahusu masuala
mengi yaliyo katika
mwongozo huu. Kanisa lilipokuwa linakua kwa kasi ulimwenguni kote mwanzoni
mwa karne ya ishirini, lilizidi kutambua hitaji la kuwa
na mwongozo kwa ajili ya
kutumiwa na wachungaji na washiriki wake walei ulimwenguni kote. Mwaka
1931 Kamati ya Konferensi Kuu iliamua kuchapisha mwongozo wa kanisa. J. L.
McElhany, ambaye baadaye alikuwa mwenyekiti wa Konferensi Kuu,
aliandaa muswada, ambao ulichapishwa mwaka 1932.Sentensi ya kwanza ya
utangulizi wa toleo hilo la kwanza ilikuwa inasema, “imedhihirika zaidi
kwamba unahitajika mwongozo wa uendeshaji wa kanisa ili kuelezea na
kuhifadhi desturi na taratibu za dhehebu letu.” Zingatia neno kuhifadhi.
Hili halikuwa jaribio la kuunda na kushinikiza haraka utaratibu mzima wa
utawala kanisani. Bali ilikuwa juhudi ya kwanza ya kuhifadhiuamuzi
wote mzuri uliokuwa unafanyika katika miaka yote na kisha
14
kuongeza kanuni
zinazohitajika kwa ajili ya ukuaji na uchangamano wa Kanisa uliokuwa
unaongezeka Mamlaka na Kazi ya Mwongozo wa Kanisa Mwongozo wa Kanisaumekuwa
katika mfumo wa sasa tangu mwaka 1932. Unaelezea shughuli na kazi za
makanisa mahalia na uhusiano wa makanisa hayo na ngazi zingine za Kanisa
ambako yana ushirika. Vilevile, Mwongozo wa Kanisaunaelezea jinsi Kanisa
linavyoyaelewa maisha ya Kikristo na uendeshaji na nidhamu ya Kanisa kwa
kufuata kanuni za Biblia na mamlaka ya Mikutano rasmi ya Konferensi Kuu.
“Mungu ameagiza kwamba, wawakilishi wa kanisa lake kutoka pande zote za
dunia, wakikutana katika Konferensi Kuu, watakuwa na mamlaka.”—9T 261. Mwongozo
wa Kanisaumegawanyika katika sehemu mbili. Yaliyomo katika kila sura ni
kwa ajili ya kila taasisi ya kanisa, kanisa mahalia, na kila mshiriki. Kwa
kutambua haja ya kuwa na tofauti katika sehemu kadhaa, maelezo ya
nyongeza, yaliyotolewa kama mwongozo na vielelezo, yapo mwishoni mwa
Mwongozo huu wa Kanisa. Maelezo haya yana na vichwa vidogo
vinavyokwenda sambamba na vichwa vidogo vya sura na kurasa za matini ya
msingi.Viwango na desturi za Kanisa zimejengwa katika kanuni za Maandiko
Matakatifu. Kanuni hizi, zinazosisitizwa na Roho ya Unabii, zimeelezewa
katika Mwongozo huuwa Kanisa. Hazina budi kufuatwa katikamasuala yote
yanayohusu utawala na uendeshaji wa makanisa mahalia. Mwongozo wa
Kanisapia unafafanua uhusiano kati ya kanisa mahalia na konferensi mahalia
au vyombo vingine katika muundo wa dhehebu la Waadventista wa Sabato.
Hairuhusiwi kujaribu kuweka viwango vya ushirika au kujaribu kutunga au
kutumia, kanuni na taratibu kwa ajili ya uendeshaji wa kanisa mahalia
zilizo kinyume na uamuzi huu uliopitishwa katika kikao cha Konferensi Kuu
na ambao umeelezewa katika Mwongozo huu wa Kanisa.Kufanya MabadilikoKwa
miaka mingi Konferensi Kuu imekuwa ikipitisha mabadiliko muhimu katika
Mwongozo wa Kanisa. Kwa kutambua
15
umuhimu wa kuendesha
kazi ya Kanisa ulimwenguni kote “kwa uzuri na kwa utaratibu,”katika kikao
chake cha mwaka 1946, Konferensi Kuu iliamua kwamba “mabadiliko na
masahihisho ya sera yatakayofanyika katika Mwongozo huu yataidhinishwa
na kikao cha Konferensi Kuu.” General Conference Report,No. 8 uk.197
(Juni 14, 1946).
Kwa kutambua kuwa wakati
mwingine hali ya sehemu fulani huhitaji uamuzi maalum, mwaka 1948 Kamati
ya Konferensi Kuu iliamua kwamba “kila divisheni duniani, ikiwemo
Divisheni ya Kaskazini mwa Amerika, iandae ‘Nyongeza’ ya Mwongozo mpya
wa Kanisabila kuubadilisha kwa namna yo yote ile bali uwe na nyongeza inayohusu
hali iliyopo katika divisheni husika; rasimu za nyongeza hizo hazina budi
kuwasilishwa katika Kamati ya Konferensi Kuu ili zipitishwe. – Autumn
Council Actions, 1948, uk. 19.Kikao cha Konferensi Kuu cha mwaka 2000,
kiliidhinisha kuainishwa upya kwa baadhi ya maelezo yaliyo katika
Mwongozo wa Kanisa, na kuyaweka katika sehemu ya Maelezo kama maelekezo
na mifano badala ya kuwa mambo ya lazima; pia kiliidhinisha mchakato wa kufanya
mabadiliko. Mabadiliko katika Mwongozo wa Kanisa,isipokuwa katika sehemu
ya maelezo na mabadiliko yatokanayo na uhariri, yanaweza kufanywa
kwa uamuzi wa kikao cha Konferensi Kuu tu, ambapo wajumbe wa kanisa
la ulimwengu wanaweza kutoa maoni na kupiga kura. Kama kanisa mahalia,
konferensi, misheni ya konferensi/union inataka kupendekeza marekebisho ya
Mwongozo wa Kanisa, haina budi kuwasilisha pendekezo lake kwa ngazi
inayofuata kwa ajili ya ushauri na uchunguzi. Kama ngazi hiyo italipitisha
pendekezo hilo, itawasilisha mabadiliko yaliyopendekezwa kwa ngazi
inayofuata kwa ajili ya tathmini zaidi. Kama ngazi mbalimbali
zitalipitisha pendekezo hilo, hatimaye litafika kwenye Kamati ya Mwongozo
wa Kanisaya Konferensi Kuu, ambayo huyachunguza mapendekezo yote.
Kama Kamati ya Mwongozo wa Kanisaitayapitisha mabadiliko hayo,
itayaandaa kwa ajili ya kuyawasilisha kwenye Baraza la Mwaka na/au kikao
rasmi cha Konferensi Kuu.Mabadiliko ya maelezo hufuata utaratibu huo huo.
Kamati Tendaji ya Konferensi Kuu inaweza kupitisha mabadiliko ya maelezo
katika Kikao cho chote cha Baraza la Mwaka.
16
Kamati ya Mwongozo wa
Kanisaitawasilisha taarifa ya mabadiliko yaliyopendekezwa, yatokanayo na
uhariri, ambayo hayabadili maana katika Mwongozo wa Kanisa, kwenye
Baraza la Mwaka la Kamati Kuu ya Utendaji ya Konferensi Kuu,
ambalo linaweza kuyaidhinisha. Hata hivyo, Baraza la Mwaka
likiamua kwa theluthi moja ya kura, kuwa badiliko hilo la kiuhariri
limebadili maana ya ibara husika, basi badiliko hilo
lililopendekezwa litapelekwa kwenye kikao cha Konferensi Kuu. Katika
Baraza la Mwaka wa mwisho wa kipindi cha miaka mitano, Kamati Tendaji ya
Konferensi Kuu itapitia mabadiliko yote katika maelezo na kuoanisha
mabadiliko hayo na marekebisho yo yote yanayoweza kuwa yamependekezwa
katika sehemu ya msingi ya Mwongozo wa Kanisa.
Toleo jipya la Mwongozo
wa Kanisahuchapishwa kila baada ya kikao cha Konferensi Kuu. Toleo jipya
kuliko yote halina budi kutumika kila wakati. Toleo hili lina marekebisho
yaliyofanywa kwenye kikao cha Konferensi Kuu cha mwaka 2010. Mahali pa
Kupata Ushauri Maofisa wa kanisa na viongozi,
wachungaji, na washiriki hawana budi kuwasiliana na
konferensi zao kwa ajili ya ushauri juu ya uendeshaji wa makanisa yao au
masuala yanayotokana na Mwongozo huu wa Kanisa. Kama hawatakubaliana,
itabidi wawasiliane na misheni/konferensi ya union kwa ajili ya ufafanuzi.
Istilahi Zilizotumika katika Mwongozo huu wa Kanisa Kanisa—Kwa sababu za
kiuhariri na kiuchapaji, neno “Kanisa,” linapoanza na “K” kubwa katika
kitabu hiki, litakuwa limetumika badala ya jina kamili la “Kanisa la
Waadventista wa Sabato” na litamaanisha muundo mzima wa Kanisa na si
kanisa mahalia au kundi, isipokuwa linapotumika katika dondoo. Konferensi,
misheni, seksheni, ujumbe, field, umoja
wa makanisa– Kwa sababu za kiuhariri na kiuchapaji, katika
kitabu
hiki “konferensi”
inamaanisha “konferensi, misheni, field, seksheni,
ujumbe, au umoja wa makanisa,” kulingana na muktadha
17
wa kiutawala. Kwa
ujumla, kila kanisa ni sehemu ya jumuiya ya makanisa ijulikanayo kama
konferensi, lakini kabla jumuiya hiyo haijawa na hadhi ya konferensi,
kulingana na Sera ya Uendeshaji ya Konferensi Kuu, inaweza kuitwa misheni,
seksheni, ujumbe, au field. Katika baadhi ya divisheni ulimwenguni,
jumuiya za makanisa katika nchi fulani hufanya kazi kama konferensi kwa
shughuli za makanisa mahalia na kama union kwa shughuli zingine za
kimuundo wa Kanisa. (Tazama Sura ya 3, “Muundo na Mamlaka.”) Mchungaji—Wachungaji
wanaotajwa ndani ya kanuni hii ni wale walioteuliwa na konferensi
kusimamia mambo ya kanisa mahalia au mtaa. Vifupisho vya vitabu vya Ellen
G. White vimeelezewa katika uk. 179. Madondoo ya Maandiko yanatoka
katika Biblia ya Kiswahili, Toleo la Union isipokuwa pale
ilipoelezwa vinginevyo.
18
SURA
2
Kanisa la Mungu Aliye
Hai Maandiko hutumia usemi kama “kanisa lake Mungu” (Mdo. 20:28), “mwili
wa Kristo” (Efe. 4:12), “kanisa la Mungu aliye hai” (1 Tim. 3:15). Kuwa
sehemu ya kanisa la Mungu ni fursa ya pekee na ya kuridhisha moyo. Kusudi
la Mungu ni kukusanya watu kutoka pande za mbali za dunia ili
kuwaunganisha katika mwili mmoja, yaani mwili wa Kristo, ambapo yeye ni
kichwa kilicho hai. Wote walio watoto wa Mungu katika Kristo Yesu ni
viungo vya mwili
huu, na katika uhusiano
huo wanaweza kunufaika na ushirika kati yao, na kuwa na ushirika na Bwana
wao pia. Biblia imetumia neno “kanisa” kwa namna zisizopungua mbili: kwa
maana ya jumla likimaanisha kanisa ulimwenguni kote (Mat. 16:18; 1
Kor.12:28), na pia kwa maana mahususi likimaanisha kanisa katika mji au
jimbo, kama vile kwa wote walioko Rumi (Rum. 1:6, 7), Korintho (1 Kor.
1:2), na Thesalonike (1 Thes. 1: 1), na Galatia (1 Kor. 16:1), Asia (1
Kor. 16:19), na Shamu na Kilikia (Mdo. 15:41).
Kristo, akiwa kichwa cha
kanisa na Bwana wake aliye hai, ana upendo mkubwa kwa viungo vya mwili
wake. Inampasa kutukuzwa katika kanisa (Efe. 3:21); ataidhihirisha “hekima
ya Mungu iliyo ya namna nyingi” (Efe. 3: 10) kwa njia ya kanisa. Yeye
hulilisha na kulistawisha kanisa lake siku kwa siku (Efe. 5:29), na shauku
yake ni kulifanya liwe “kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi,
wala lolote kama hilo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Efe. 5:27).
Hakuna Kiambaza
Kinachotutenga Kristo alijitahidi, kwa mafundisho na mfano, kufundisha
ukweli kwamba kwa Mungu haikupasa kuwe na kiambaza kati ya Israeli
na mataifa mengine (Yn.
4:4-42; 10:16; Lk. 9:51-56; Mat. 15: 21-28). Mtume Paulo aliandika, “Mataifa ni
warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja na washiriki pamoja
nasi wa
19
ahadi yake iliyo katika
Kristo Yesu kwa njia ya injili” (Efe. 3:6). Wala haipasi kuwa na upendeleo wa
tabaka au taifa au jamii au rangi, miongoni mwa wafuasi wa Kristo, kwani
wote ni wa damu moja. Wateule wa Mungu, jamii ya ulimwengu mzima, jamii
mpya ya wanadamu, wote wamekuwa “mmoja katika Kristo Yesu” (Gal. 3:28).
“Kristo alikuja katika dunia hii akiwa na ujumbe wa rehema na msamaha. Aliweka
msingi wa dini ambapo Wayahudi na Watu wa Mataifa, weusi na weupe, walio
huru na watumwa, wameunganishwa katika udugu wa pamoja, wakitambuliwa
kuwa wako sawa machoni pa Mungu. Mwokozi ana upendo usio na kikomo
kwa kila mwanadamu.”—7T 225. “Hakuna tofauti inayotambuliwa na Mungu kwa
sababu ya
utaifa, rangi, au
tabaka. Yeye ndiye Mwumbaji wa wanadamu wote. Wanadamu wote ni wa familia
moja kutokana na kuumbwa, na wote ni wamoja kwa njia ya ukombozi. Kristo
alikuja kubomoa kila kiambaza kinachotutenga, kuzifungua hema zote za
hekalu, ili kila mtu aweze kumfikia Mungu. ... Katika Kristo hakuna
Myahudi wala Myunani, hakuna mtumwa wala aliye huru. Wote huvutwa kwa
damu yake ya thamani.” — COL 386.
Kitu Ambacho Kristo
Anakijali Kuliko VyoteWale walio katika kazi ya Kristo, walioitwa kuwa
viongozi, inawapasa “kulitunza kanisa” (1 Tim. 3:5); inawapasa
“kulilisha kanisa lake Mungu” (Mdo. 20:28); na kuwa na “maangalizi
ya makanisa yote” (2 Kor. 11:28). “Nawashuhudia ndugu zangu kwamba
kanisa la Kristo, japo ni
dhaifu na lenye kasoro
sana, ni kitu pekee anachokiangalia sana. Anapoita ulimwengu wote uje,
kwake upate kuokolewa, huwatuma malaika zake kutoa msaada wa kimbingu kwa
kila ajaye kwake kwa toba na majuto, na yeye mwenyewe huja katika kanisa
lake kwa njia ya Roho Mtakatifu.”—TM 15. Kama bibi arusi wa Kristo na
kitu anachokijali kuliko vyote, kanisa linatarajiwa kuonesha utaratibu na
tabia ya yule aliye Mungu katika shughuli zake zote. “Katika kipindi hiki
inalipasa kanisa kuvaa mavazi yake ya
20
kupendeza—‘Kristo aliye
haki yetu.’ Kuna tofauti za makusudi zilizo wazi ambazo hazina budi
kurejeshwa na kuoneshwa kwa ulimwengu katika kuziinua amri za Mungu na
imani ya Yesu. Uzuri wa utakatifu hauna budi kuonekana katika mng’ao wake
wa asili, tofauti na uharibifu na giza la wasiotii, walioiasi sheria ya
Mungu. Kwa hiyo tunamkiri Mungu, na kuitambua sheria yake, ambayo ni msingi
wa utawala wake kule mbinguni na katika himaya zake zote duniani. Mamlaka
yake inapasa kuwekwa wazi na bayana mbele ya ulimwengu, na sheria zote
zinazopingana na sheria za Yehova hazipasi kukubalika. Ulimwengu
ukiruhusiwa kuathiri uamuzi na matendo yetu, tunapokaidi mipango ya Mungu,
makusudi ya Mungu yatakuwa yameshindwa. Hata kama sababu itakuwa ya kuvutia
sana, kanisa likiyumba katika jambo hili, katika vitabuvya mbinguni litakuwa
limeandikiwa ukosefu wa uaminifu juu ya dhamana takatifu kuliko zote
ambazo lilikabidhiwa, na udanganyifu mkubwa dhidi ya ufalme wa Kristo.
Inalipasa kanisa kushika kwa dhati kanuni zake mbele ya mbingu na falme za
ulimwengu; uaminifu usiokoma katika kulinda heshima na utakatifu wa
sheria
ya Mungu utafanya
ionekane na kuheshimiwa hata na ulimwengu, na wengi watamtukuza Baba yetu
wa mbinguni kutokana na matendo mema watakayoyaona.”—TM 16, 17.Mtume Petro
aliandika, “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu,
watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza
fadhili zake yeye
aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.” (1 Pet. 2:9).
Kamili katika Kristo“Bwana
amelipatia kanisa lake uwezo na baraka, ili liwasilishe kwa ulimwengu
taswira ya utoshelevu wake, ili liwe kamili katika yeye, yaani liwe
udhihirisho endelevu wa ulimwengu mwingine, ambao ni wa milele,
udhihirisho wa sheria ambazo ni bora kuliko sheria za duniani. Inalipasa
kanisa lake kuwa hekalu lililojengwa kulingana na mfano wa mbinguni, na
malaika ambaye ni msanifu wa majengo ameleta mwanzi wake wa dhahabu kutoka
mbinguni, ili kila jiwe lichongwe na kusafishwa lipate kung’aa kama
kielelezo cha mbingu kilivyo, likiangaza pande zote miali ya Jua la Haki.
...
21
“Bwana Yesu anaijaribu
mioyo ya wanadamu kwa kuonesha rehema na neema yake nyingi. Anafanya
mabadiliko ya ajabu ambayo Shetani, pamoja na kujigamba kwake kuwa
mshindi, pamoja na mwungano wake wa uovu ulioungana kupingana na
Mungu na sheria za serikali yake, amesimama akiyatazama
mabadiliko hayo kama ngome isiyoweza kupenyeka kwa hila na uongo
wake. Mabadiliko hayo ni fumbo kwake. Malaika wa Mungu, maserafi na
makerubi, waliotumwa kushirikiana na binadamu, wanaangalia kwa mshangao na
furaha, kwamba wanadamu walioanguka, ambao hapo awali walikuwa watoto wa
ghadhabu, wanajenga tabia zao kutokana na mafunzo ya Kristo ili zifanane
na tabia ya Mungu, na wawe wana na binti za Mungu, wafanye sehemu muhimu
katika shughuli na raha za mbinguni.“Kristo ametoa zana za kutosha kwa
kanisa lake, kusudi ajipatie utukufu mkubwa kutoka kwa milki yake
aliyoikomboa na kuinunua. Kanisa likiwa limepewa haki ya Kristo, ni hazina
yake, ambamo utajiri wa rehema yake, upendo wake, neema yake,
vitaonekana katika ukamilifu na katika udhihirisho wa mwisho.
... Katika usafi wao usiochafuliwa, na
ukamilifu usio na mawaa, Kristo anawaona watu wake kama
ujira wa mateso yake,
kudhalilishwa kwake, na
upendo wake, na nyongeza ya utukufu wake—Kristo, ambaye ni kitovu kikuu
ambapo utukufu wote hutokea. ‘Heri walioalikwa katika karamu ya arusi ya
MwanaKondoo.’”—TM 15-19. Kanisa linafuata kwa uaminifu kanuni za umoja wa
kiroho wa kanisa la Kristo zilizotajwa hapo juu. Kutokana na amani na
uwezo ambao haki ya Kristo huleta, kanisa limedhamiria kushinda kila
kizuizi ambacho dhambi
imekiweka kati ya wanadamu.
22
SURA YA 3
Muundo na Mamlaka
Muundo wa Kanisa
unatokana na kanuni za Mungu. “Msiruhusu mawazo ya mtu ye yote yayumbishe
imani yenu kuhusu utaratibu na mwafaka unaopasa kuwemo kanisani. ... Mungu
wa mbinguni ni Mungu wa utaratibu, na anataka wafuasi wake wote wawe na
sheria na kanuni, na kuhifadhi utaratibu.”—5T 274.
Msingi wa Kibiblia wa
Kuwa na MuundoMungu alipowaita wana wa Israeli kutoka Misri na
kuwachagua kuwa watu wake wa pekee, aliwapatia muundo mzuri wa
utawala kwa ajili ya kuongoza mwenendo wao katika masuala ya kiraia
na kidini.“Serikali ya Israeli ilikuwa na muundo mkamilifu kabisa, uliokuwa
mzuri katika ukamili na usahili wake. Utaratibu ambao unaonekana wazi
katika ukamilifu wa mpangilio wa viumbe vyote vya Mungu ulidhihirishwa
katika mfumo wa Waebrania. Mungu alikuwa ndiye kiini cha mamlaka na
utawala, mfalme wa Israeli.
Musa aliteuliwa na Mungu
kuwa kiongozi wao anayeonekana, ili asimamie sheria kwa niaba ya Mungu.
Baadaye lilichaguliwa baraza la watu sabini miongoni mwa wazee wa makabila
kumsaidia Musa katika mambo ya kawaida katika taifa. Baada ya hapo
kulikuwa na makuhani, waliokuwa wakiwasiliana na Mungu hekaluni.
Machifu,
au wakuu, walikuwa
wanasimamia makabila. Chini yao kulikuwa na ‘wakuu wa maelfu’, na wakuu wa
mamia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa makumi’ na mwishowe, watumishi
ambao wangeweza kupewa kazi maalumu.”—PP 374
Kanisa la Agano Jipya
lilionesha ukamilifu huo huo katika mpangilio wake. Kristo mwenyewe,
aliyeanzisha kanisa, (Mt. 16:18) “amevitia viungo kila kimoja katika mwili
kama alivyotaka” (1 Kor. 12:18). Aliwapatia karama na talanta zinazofaa
kwa kazi zilizokuwa zinawakabili, na kuwapanga kama mwili ulio
hai, utendao kazi, na yeye mwenyewe akiwa kichwa.
23
“Kwa kuwa kama vile
katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi
moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na
viungo, kila mmoja kwa mwenzake” (Rum. 12:4, 5). “Naye [Kristo] ndiye
kichwa cha mwili, yaani cha Kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa
kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote” (Kol. 1:
18).“Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena
pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.”(1 Cor. 12:4, 5) “Maana kama
vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote
vya mwili ule, navyo ni
vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.” (1 Cor. 12:4, 5)“Basi ninyi
mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu ameweka
wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu
waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na
masaidiano,
na maongozi, na aina za
lugha.” (1 Kor. 12: 27, 28). Umuhimu wa Muundo Kama vile isivyowezekana kuwa na
mwili wa mtu ulio hai na ufanyao kazi bila viungo vyake kuungana katika
mfumo na kufanya kazi pamoja, haiwezekani kuwa na kanisa hai
linalokua na kustawi bila washiriki wake kujipanga katika mwili mmoja wa kiroho,
wote wakifanya majukumu na kazi walizopewa na Mungu chini ya uongozi wa
mamlaka iliyowekwa na Mungu. Hakuna taasisi au kundi linaloweza kufanikiwa
bila ya kuwa na muundo. Bila muundo maalum, hakuna taasisi au harakati
itakayoweza
kustawi. Taifa lisilokuwa
na serikali iliyopangwa litakuwa katika machafuko. Biashara isiyokuwa na
mpangilio itaanguka. Kanisa lisilokuwa na muundo litasambaratika na
kutoweka. Kristo alilipatia kanisa lake mfumo wa muundo sahili
lakini wenye ufanisi kwa ajili ya maendeleo mema ya kanisa na kwa
ajili ya kutimiza kazi yake ya kupeleka injili ya wokovu
ulimwenguni kote. Mafanikio ya kanisa katika juhudi zake za kumaliza kazi
yake, yanategemea kufuata kielelezo hiki cha Mungu kwa
uaminifu. “Baadhi ya watu wamekuwa wakitoa wazo kuwa
kadiri tunavyokaribia mwisho wa wakati, kila mtoto wa Mungu atafanya
kazi bila kuwa katika muundo wo wote wa kidini. Lakini
24
nimeelekezwa na Bwana
kuwa katika kazi hii, hakuna suala la kila mtu kufanya kazi peke yake.”—TM
489.“Shetani atafurahi sana akifaulu katika juhudi zake kuingia miongoni
mwa watu hawa na kuivuruga kazi katika kipindi ambacho mpangilio makini ni
wa lazima na utakuwa nguvu kubwa kabisa ya kuzuia harakati za uongo na
kukanusha madai yasiyoungwa mkono na Neno la Mungu! Inatupasa kushikilia
msimamo bila kusita, ili mfumo wa muundo na mpangilio uliojengwa kwa
hekima na uangalifu mkubwa usiporomoke. Tusije, tukaruhusu
makundi yasiyo na utaratibu yanayotaka kuidhibiti kazi wakati
huu.”—TM 489.
Makusudi ya Kuwa na
Muundo“Idadi yetu ilipokuwa inaongezeka, ilionekana wazi kuwa bila muundo
wa namna fulani kungekuwa na machafuko makubwa, na kazi isingesonga mbele
kwa mafanikio. Muundo ulikuwa wa lazima kwa ajili ya kusaidia kazi ya
Mungu, kuanzisha kazi katika maeneo mapya, kulinda makanisa na kazi ya
Mungu dhidi ya washiriki wasiofaa, kutunza mali ya kanisa, kuchapisha
ukweli katika viwanda vya uchapaji, na kwa ajili ya makusudi
mengine mengi.”—TM 26.
“Kama washiriki wa
kanisa linaloonekana, na wafanyakazi katika shamba la Bwana, inawapasa wote
wanaodai kuwa Wakristo hawana budi kufanya kila liwezekanalo kudumisha
amani, mwafaka na upendo kanisani. Zingatieni ombi la Kristo: ‘Wote
wawe na umoja; kama
wewe, Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu;
ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.’ Umoja wa
kanisa ni ushuhuda wenye ushawishi kuwa Mungu amemtuma Yesu
ulimwenguni kama Mkombozi wa ulimwengu.”—5T 619, 620.
Mfano wa Agano
JipyaAgizo la Mwokozi kwa kanisa kupeleka injili ulimwenguni kote (Mt. 28:19,
20; Mk. 16:15) halikumaanisha kuhubiri injili tu, bali kuhakikisha ustawi
wa wale wanaoupokea ujumbe huo. Jambo
25
hili lilikuwa ni pamoja
na kulichunga na kulipatia kundi mahali pa kuishi, na pia kushughulikia
matatizo ya uhusiano. Hali hiyo ilikuwa inahitaji muundo. Mwanzoni, mitume
ndio walikuwa baraza lililokuwa linaongoza shughuli za kanisa likiwa
Yerusalemu (Mdo. 6:2; 8:14). Kundi hilo lilipokuwa kubwa kiasi cha
uendeshaji wa mambo yake kuwa mgumu, kanisa lilichagua mashemasi kwa ajili
ya kusimamia
shughuli zake (Mdo.
6:2-4).
Baadaye, makundi mengine
yakakua, si Asia tu, bali hata Ulaya, na jambo hili lilihitaji hatua zaidi
za muundo. Kule Asia Ndogo, wazee walichaguliwa “katika kila kanisa” (Mdo.
14:23). Kupanuka kwa kazi katika majimbo mbalimbali ya Dola ya Kirumi
kulihitaji kuyapangilia makanisa katika kile kinachoweza kuitwa
konferensi
(Gal. 1:2). Kwa njia
hiyo, muundo ukawa unaongezeka hatua kwa hatua katika kanisa la awali.
Kadiri kulivyokuwa na mahitaji, Mungu alikuwa anawaelekeza viongozi wa
kazi yake kwa namna ambayo, kwa kushauriana na kanisa, walijenga mfumo
ambao
ulikuwa unalinda maslahi
ya kazi.Muundo wa Sasa wa Kanisa Mfumo wa uongozi wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato ni wakilishi, unaozingatia kuwa mamlaka yako kwa
washiriki na yanadhihirishwa kwa kutumia wawakilishi katika kila
ngazi ya muundo, ambapo majukumu ya utendaji hukasimiwa kwa vyombo
wakilishi na maofisa kwa ajili ya uendeshaji wa Kanisa katika kila ngazi.
Mfumo huu wa utawala unatambua pia kuwa kuwekewa mikono kwa ajili ya
huduma kunatambuliwa na Kanisa ulimwenguni kote. “Kila mshiriki
wa kanisa ana haki ya kuchagua maofisa
wa kanisa. Kanisa huchagua maofisa wa konferensi.
Wajumbe waliochaguliwa
na konferensi huchagua maofisa wa
union, na wajumbe waliochaguliwa
na union huchagua maofisa wa Konferensi Kuu.
Kwa utaratibu huu, kila konferensi, kila taasisi, kila kanisa, na kila
mtu, hupata haki ya kuchagua watu wanaobeba majukumu makubwa ya Konferensi
Kuu, ama moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi.”—TM 236, 237.
26
Mfumo wa kimuundo uliopo
katika Kanisa ulitokana na ufahamu wa kiteolojia wa kazi ya Kanisa,
ongezeko la washiriki, na kuenea kwa Kanisa kijiografia.
Wawakilishi wa konferensi walikutana mwaka 1863 kuunda
Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato.Kuna ngazi mbalimbali katika Kanisa
kuanzia muumini mmoja mpaka mahali ambapo kazi ya ulimwengu mzima
hupangiliwa. Makundi ya washiriki katika kila ngazi hukutana mara kwa
mara katika mikutano rasmi ya kujadili shughuli za kanisa ijulikanayo kama
vikao. (Kikao cha kanisa mahalia kwa kawaida huitwa Mkutano Mkuu wa
Kanisa.) Katika muundo wa Kanisa la Waadventista wa
Sabato, hakuna ngazi
inayoweza kuamua yenyewe iwe daraja gani wala kufanya kazi kana kwamba
haiwajibiki kwa familia ya Kanisa iliyo nje ya mipaka yake.
Ngazi za Muundo wa
Kanisa
1. Kanisa Mahalia—Kundi
la washiriki walio katika eneo mahususi lililopewa daraja rasmi kama
kanisa na kikao cha konferensi.
2. Konferensi
Mahalia—Muungano wa makanisa mahalia, katika eneo mahususi la kijiografia,
uliopewa daraja rasmi la konferensi mahalia ya Waadventista wa Sabato
kwa uamuzi wa kamati kuu ya divisheni katika kikao cha katikati ya mwaka,
mwishoni mwa mwaka, au mkutano wa Baraza la Divisheni, na
hatimaye kukubaliwa na kikao cha Union kuwa sehemu ya jumuiya ya
konferensi/misheni. (tazama uk. 20.)
3. Umoja wa Makanisa—Ni
muungano wa makanisa, yaliyo katika eneo mahususi
la kijiografia, ambao umepewa, na kikao cha Konferensi
Kuu, daraja rasmi la umoja wa wakanisa ulio na hadhi ya konferensi
au misheni.
4. Konferensi/Misheni ya
Union—Ni muungano wa konferensi katika eneo mahususi la kijiografia,
ambao umepewa daraja rasmi la konferensi/misheni ya union na kikao
cha Konferensi Kuu.
27
5. Konferensi Kuu na
Divisheni zake—Konferensi Kuu inawakilisha sauti ya Kanisa ulimwenguni
kote. Jumuiya zake zimeelezewa katika katiba yake. Ili
kurahisisha shughuli zake ulimwenguni kote, Konferensi Kuu imeweka
ofisi za kanda, zinazojulikana kama divisheni za Konferensi Kuu, ambazo
zimepewa, na mabaraza ya mwaka ya Kamati Tendaji ya Konferensi Kuu,
wajibu wa kusimamia utawala wa kawaida wa muungano wa makundi ya
union na vitengo vingine vya Kanisa katika
maeneo mahususi ya
kijiografia.
6. Biblia ni msingi na
chanzo cha imani na mwenendo; kwa msingi huo, kikao cha Konferensi Kuu
katika Mkutano wake Mkuu huwa kinabainisha imani za msingi za Kanisa.
Vilevile, kikao cha Konferensi Kuu huidhinisha kuundwa kwa union na
kuambatanisha field, hurekebisha Mwongozo wa Kanisa, huchagua viongozi
wa Konferensi Kuu na wa divisheni, hufanya shughuli nyingine kama
zilivyoelezwa kwa ufupi katika Katiba na Sheria Ndogo, na hujadili
mambo yaliyowasilishwa na Kamati Kuu. Katikati ya vikao
vya Konferensi Kuu, Kamati Tendaji ya Konferensi Kuu inaruhusiwa na
Katiba pamoja na Sheria Ndogo Ndogo, kufanya kazi kwa niaba ya maeneo
mbalimbali. Kwa hiyo, jumuiya za Kanisa duniani kote
zinakitambua kikao cha Konferensi Kuu kuwa ndiyo sauti ya Kanisa.
Wajibu wa TaasisiNgazi
mbalimbali za kanisa huwa zinaendesha taasisi anuwai za elimu, afya,
uchapishaji na zingine zinazohudumia watu katika jina la Kristo kukidhi
mahitaji ya ulimwengu uliojaa fadhaa. Katika teolojia na falsafa ya
Waadventista wa Sabato, taasisi hizi tangu zilipoanzishwa zimekuwa nyenzo
muhimu katika kutimiza kazi ya kiroho ya Kanisa ya kumhudumia mwanadamu
katika ujumla wake na kupeleka injili ulimwenguni. Hakuna jumuiya au
taasisi ya Kanisa itakayobeba jukumu kwa ajili ya dhima, madeni, makosa ya
kutenda au kutotenda ya jumuiya
28
nyingine ya Kanisa eti
kwa sababu ya kushirikishwa kwake katika kanisa. Mamlaka katika Kanisa la
AwaliKama Mwumbaji, Mkombozi na Mruzuku, Bwana na Mfalme wa viumbe vyote,
Mungu pekee ndiye chimbuko la mamlaka ya Kanisa. Alikasimu mamlaka kwa
manabii wake na mitume (2 Kor. 10:8). Hivyo, walikuwa wanashika nafasi
muhimu sana na ya pekee katika kueneza Neno la Mungu na kulijenga kanisa
(Efe. 2:20).Kanisa la awali lilikuwa linawajibika na usafi wa mafundisho
na mwenendo. Wazee (au maaskofu) walikuwa na mamlaka makubwa.
Moja kati ya kazi zao
kubwa ilikuwa mafunzo ya kawaida ya kichungaji (Mdo. 20:17-28; Ebr. 13:17;
1 Pet. 5:1-3), pamoja na kazi maalum kama vile kufundisha mafundisho
sahihi na kubainisha uongo wa wale waliokuwa wanayapinga (1 Tim. 3: 1, 2;
Tit. 1:5,9). Waliambiwa hivi “zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana
na Mungu” (1 Yoh. 4:1) au, kwa usemi wa Paulo, “jaribuni mambo yote”
na “lishikeni lililo jema” (1 The.5:21).Ndivyo ilivyokuwa katika kutoa marudi
(Mt. 18:15-17), yaliyokuwa yanaanzia katika maonyo binafsi na ya malezi (linganisha
na Mt. 18: 16; Gal. 6:1) hadi kuondolewa katika ushirika (Mt. 18:18; 1
Kor. 5:11, 13; 2 Kor. 2:5-11).Kwa hiyo Kanisa lina mamlaka ya kuamua juu ya
kanuni za uendeshaji wake.Konferensi Kuu ni Mamlaka ya Juu Kuliko ZoteLeo
hii katika Kanisa, kikao cha Konferensi Kuu, na Kamati Tendaji ya
Konferensi Kuu katikati ya vikao vya Konferensi Kuu, ndiyo mamlaka ya juu
kabisa ya kikanisa, katika uendeshaji wa Kanisa. Kamati Tendaji ya
Konferensi Kuu inaruhusiwa na katiba yake kuunda taasisi ndogo ndogo zenye
mamlaka ya kutekeleza majukumu ya taasisi hizo. Kwa hiyo, jumuiya zote
zilizo chini yake na taasisi zote katika Kanisa zitakitambua kikao cha
Konferensi Kuu, na Kamati Tendaji ya Konferensi Kuu katikati ya vikao
vya
Konferensi Kuu, kama
mamlaka ya juu kabisa ya kikanisa, iliyo
29
chini ya Mungu, miongoni
mwa Waadventista wa Sabato.Kukitokea kutokuelewana kati ya makanisa na
konferensi au taasisi, kukata rufaa katika ngazi inayofuata ni sahihi
hadi itakapofika katika Baraza la Mwaka la Kamati
Tendaji ya Konferensi Kuu au kikao cha Konferensi Kuu.
Katikati ya vikao hivyo, Kamati Tendaji ya Konferensi Kuu itakuwa chombo
chenye mamlaka ya mwisho katika masuala yote. Uamuzi wa kamati
hiyo unaweza kubadilishwa katika kikao cha Konferensi Kuu au
Baraza la Mwaka. Jumuiya zinapopitia upya uamuzi wa jumuiya
nyingine, haziwajibiki na dhima ya jumuiya nyingine yo yote ile.“Mara kwa
mara nimeelekezwa na Bwana kuwa hakuna uamuzi wa mtu ye yote unaopasa
kusalimishwa kwa uamuzi wa mtu mwingine ye yote. Mawazo ya mtu mmoja au ya
watu wachache yasichukuliwe kuwa yanatosha katika hekima na uwezo
wa kuendesha kazi, na kuamua mipango ya kufuatwa. Lakini, uamuzi wa
ndugu waliokusanyika toka sehemu zote za kanisa unapofanyika katika
‘Konferensi Kuu,’ uhuru binafsi na uamuzi binafsi haupaswi kuendelezwa
kikaidi, bali uachwe. Mtenda kazi ye yote asichukulie kuwa jambo jema
kung’ang’ania maoni yake ya binafsi, dhidi ya uamuzi wa chombo hicho kikuu.” –
Testimonies for the Church, Kitabu cha 9 uk 260.
30
SURA YA 4
Wachungaji na Watumishi Wengine wa Kanisa
Kazi Aliyoagiza Mungu
“Mungu ana kanisa, nalo lina kazi ambayo limeagizwa na Mungu. ‘Naye alitoa
wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti; na
wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,
hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na
sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa
Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu hata kufika kwenye cheo cha kimo cha
utimilifu wa Kristo. ...’“Watu walioteuliwa na Mungu wamechaguliwa
ili walinde kwa uangalifu wenye wivu, na saburi iliyojaa tahadhari
ili kanisa lisiangushwe na hila mbaya za Shetani, bali lisimame katika
ulimwengu kwa ajili ya kuendeleza utukufu wa Mungu miongoni mwa watu.”—T9
52, 53. Mwenyekiti wa Konferensi—Mwenyekiti wa konferensi hana budi kuwa
mchungaji aliyewekewa mikono, mwenye uzoefu na sifa njema. Ni msimamizi wa
kazi ya injili katika konferensi na ni mzee
kiongozi au mwangalizi
wa makanisa yote. Hushughulikia ustawi wa kiroho wa makanisa hayo na
kuyashauri kuhusu shughuli na mipango yao. Ana haki ya kwenda katika
makanisa yote na katika huduma zao, vikao vya mkutano mkuu, pamoja na
mabaraza bila kuwa na haki ya kupiga kura kama hajaruhusiwa na kanisa,
au kama si mshiriki wa kanisa hilo. Ikibidi anaweza kuwa
mwenyekiti wa kikao cho chote cha kanisa lo lote. Ana haki ya kuona
nyaraka zote za kanisa. Mwenyekiti wa konferensi hana mamlaka ya
kuondoa maofisa wa kanisa waliochaguliwa kihalali lakini atafanya kazi kwa
31
kushirikiana nao. Nao
kwa upande wao, wakitambua mshikamano wa ushirika wa konferensi,
wanatakiwa kushauriana naye, katika mambo yote yanayohusu ustawi wa
kanisa. Wasijaribu kumtenga katika utekelezaji halali wa kazi
zake.Wakurugenzi wa Idara wa Konferensi—Wakurugenzi wa idara wa Konferensi
huhamasisha maeneo muhimu sana ya kazi ya kanisa chini ya uongozi wa
kamati ya konferensi ikishauriana na mwenyekiti wa konferensi. Ili wafanye
kazi waliyopewa kwa ufanisi, watumishi hawa lazima wawe na fursa ya
kwenda makanisani kuwasilisha na kutengeneza mipango yao.
Inawapasa watumishi hawa kuzingatia mipango yote ya kanisa, hata iliyo
nje, ya idara zao.Wakurugenzi wa idara hawana mamlaka ya utawala au
utendaji, kwa hiyo uhusiano wao na makanisa mahalia ni wa kutoa
ushauri. Kazi yao haina uhusiano na makanisa kama ule wa kamati
ya konferensi au wa mwenyekiti. Katika kuhamasisha aina mahususi za
kazi zao, huwa wanafanya kazi katika konferensi nzima. Hata hivyo,
hawategemewi kuyashauri makanisa kuhusu uchaguzi na majukumu mengine ya kiutawala
au maeneo mengine ya kazi, kama hawajaagizwa kufanya hivyo na
mwenyekiti. Wachungaji Waliowekewa Mikono—Wachungaji
waliowekewa mikono walioteuliwa na kamati ya konferensi kuwa wachungaji
au viongozi wa mitaa hawachukui nafasi ya mwenyekiti katika
maeneo yao. Hawana mamlaka ya kiutawala kama alivyo mwenyekiti,
bali hushirikiana naye katika kutekeleza mipango na sera za konferensi. Mchungaji
aliyewekewa mikono akipangwa kwenye kanisa mahalia, husaidiwa na wazee
mahalia. Kwa sababu ya kuwekewa mikono, mchungaji anaweza kuhudumu katika
kaida za dini na huduma maalum. Inampasa mchungaji kuwa kiongozi na
mshauri
wa kiroho wa kanisa
lake. Wachungaji hawana budi kuwaelekeza maofisa katika katika
kazi zao na kupanga pamoja nao
katika maeneo yote ya kazi na shughuli za kanisa. Mchungaji ni
mjumbe wa baraza la kanisa na ndiye mwenyekiti wake. Mchungaji akitaka
kupunguziwa jukumu la kuwa mwenyekiti wa baraza, mzee wa kanisa huwa
mwenyekiti akishirikiana na
32
mchungaji. (taz. uk.
72.) Mchungaji, akisaidiwa na wazee wa kanisa, anategemewa kupanga na
kuongoza huduma zote za kiroho, kama vile ibada ya Siku ya Sabato na
mikutano ya maombi, na inampasa kuendesha huduma ya meza ya Bwana na
ubatizo. Wachungaji wasiwe na kundi la washauri wa kujichagulia, bali
washirikiane na maofisa waliochaguliwa. Kunapokuwa na mwinjilisti
aliyeombwa kufanya mkutano wa injili katika eneo lenye kanisa, konferensi
haina budi kumwalika mchungaji kumsaidia mwinjilisti, ili kumpa mchungaji
fursa ya kuwafahamu washiriki watarajiwa.Wachungaji au wachungaji
wasaidizi hawapendekezwi au kuteuliwa kushika nafasi hizo na kanisa.
Uhusiano wao na kanisa unatokana na uteuzi wa kamati ya konferensi, na
uteuzi huo unaweza kubadilishwa wakati wo wote. (tazama uk. 73) Mchungaji
anaweza kuondolewa kazini kwa uamuzi wa kamati ya konferensi bila kuathiri
ushirika wake. Lakini, mchungaji akiondolewa katika ushirika wa kanisa na
baadaye kurudishwa katika ushirika kama mlei, kurejeshwa kwa ushirika
wake hakumaanishi kurejeshwa katika utumishi.Wachungaji wenye Leseni—Ili
kuwapa watu fursa ya kuonesha wito wao katika utumishi, hususan katika
uongoaji wa roho, wataradhia wa kazi hiyo hupewa leseni ya uchungaji na
konferensi. Kutolewa kwa leseni hizo huwapatia fursa ya kukuza karama ya uchungaji.
Wachungaji wenye leseni wana mamlaka ya kuhubiri, kufanya uinjilisti,
kuongoza katika kazi ya umisionari, na kusaidia katika shughuli zote za
kanisa. Hata hivyo, kuna mazingira, ambapo huilazimu konferensi kuteua
mchungaji mwenye leseni kubeba jukumu la mchungaji au mchungaji msaidizi
wa kanisa au jumuiya ya makanisa. Ili kumwezesha mchungaji mwenye leseni
kufanya kazi fulani za kichungaji, inabidi kanisa au kundi la makanisa
anayoyahudumia yamchague mchungaji huyo kuwa mzee wa kanisa mahalia. Baada
ya hapo, kwa kuwa uwezo
wa kuruhusu kuongezwa kwa madaraka ya mchungaji mwenye leseni ni wa kamati
kuu ya divisheni, inapasa kamati hiyo iidhinishe ongezeko hilo la mamlaka
kwa
33
kubainisha kazi za ziada
ambazo mchungaji huyo mwenye leseni anaweza kuzifanya. Kazi hizo za ziada
ni katika kanisa au kundi la makanisa ambapo mchungaji huyo mwenye leseni
anafanyia kazi na ni mzee wa kanisa. Baada ya kamati ya divisheni kuamua, kamati
ya konferensi sasa inaweza kuchukua hatua. (tazama uk. 74) Kamati ya konferensi
haitaongeza kazi za mchungaji mwenye leseni zaidi ya zile zilizoruhusiwa
na kamati ya divisheni. Pia haitamruhusu mchungaji mwenye leseni
kufanya kazi zilizoongezwa katika kanisa lo lote nje ya mahali ambapo
amechaguliwa kama mzee wa kanisa. Uamuzi wa Kamati ya konferensi
hauwezi kuwa badala ya uchaguzi wa kanisa au kuwekewa mikono kwa
ajili ya kazi ya injili. Walimu wa Biblia—Konferensi inaweza kuajiri walimu
wa Biblia na kuwapa kazi katika mikutano ya injili au makanisa
na makundi mahalia. Pamoja na kwamba walimu hawa hufanya kazi chini
ya konferensi kwa ujumla, mwalimu wa Biblia anayefanya kazi
katika mkutano wa injili
atakuwa chini ya uongozi wa mwinjilisti anayeendesha mahubiri hayo, na
mwalimu anayefanya kazi katika kanisa atakuwa chini ya uongozi wa
mchungaji. Mwalimu wa Biblia haruhusiwi kupewa kazi katika kanisa mahalia
isipokuwa kwa makubaliano maalum na konferensi, bali inapasa awe
huru kufanya kazi ya kuongoa roho.
Konferensi Husimamia
Watumishi wa Kanisa—Mwenyekiti wa konferensi, kwa kushauriana na kamati ya
konferensi husimamia watumishi wote wa konferensi kama vile wachungaji,
walimu wa Biblia, na wakurugenzi wa idara, ambao hupata
vitambulisho kutoka konferensi na huwajibika kwa konferensi, na si kwa
kanisa mahalia. Kanisa linaweza kumwomba mwenyekiti wa
konferensi lipate huduma au msaada wa watumishi wa konferensi,
lakini kwa hali yo yote ile, uteuzi utafanywa na kamati ya
konferensi. Kamati ya konferensi inaweza kubadili kazi za watumishi
wakati wowote inapoona kuwa zinahitajika. Mtumishi au kanisa anaweza kukata
rufaa kwa kamati ya konferensi ili kuupima uamuzi wa kuhamishwa kwa
mtumishi husika na kamati itaiangalia rufaa hiyo
34
kwa makini ikizingatia
mahitaji ya konferensi nzima. Mtumishi akikataa kushirikiana na kamati na
kukataa kutekeleza uamuzi wa kamati, kamati inaweza kuuchukulia mwenendo
wa mtumishi huyo kama ukaidi na inaweza kuushughulikia ipasavyo. Kwa namna
yo yote ile, mtumishi haruhusiwi kukata rufaa kwa kanisa
kuhusu uamuzi kama huo. Kanisa likiunga mkono ukaidi wa
mtumishi, nalo litastahili marudi kutoka konferensi.
Vitambulisho na Leseni
Kazi ya Mungu haina budi
kulindwa kwa wivu na viongozi wawajibikaji kuanzia katika kanisa mahalia
hadi Konferensi Kuu. Vitambulisho na leseni rasmi hutolewa kwa watumishi
wote wa kudumu walioidhinishwa, navyo hutolewa na kamati za
utawala kwa vipindi maalum.
Katika konferensi
mahalia, kamati hutoa mamlaka kwa watu kuliwakilisha Kanisa kama
wachungaji na wahudumu wa injili. Mamlaka hayo hutolewa kwa kuwapatia
vitambulisho na leseni, ambavyo ni maagizo yaliyoandikwa yakiwa na tarehe
na kusainiwa ipasavyo na viongozi wa konferensi. Mamlaka inayotolewa kwa
njia hiyo, si ya mtu na haitokani na mtu bali ni ya chombo
kilichoitoa, ambacho kinaweza kuagiza vitambulisho hivyo
virudishwe wakati wo wote, kama aliyepewa atakiuka masharti ya kazi
yake. Vitambulisho na leseni si mali yao binafsi na inapasa
virudishwe ajira inapositishwa au vikitakiwa na taasisi
iliyovitoa. Ili maadui wa Kanisa wasitumie mimbari zetu, mtu ye yote
asiruhusiwe kuhutubia mkutano wo wote wa kanisa asipoonesha kitambulisho
au leseni hai ya kanisa. Hata hivyo, inaeleweka kuwa wakati
mwingine makanisa yanaweza kuhutubiwa na viongozi wa serikali; lakini watu
wote wasioidhinishwa wasiruhusiwe kutumia mimbari.
Vitambulisho na Leseni
Zilizomaliza Muda Wake—Vitambulisho na leseni hutolewa kwa kipindi maalum kama
inavyoelezwa katika katiba ya konferensi pamoja na sheria ndogo ndogo au
sera ya uendeshaji, na huwa zinatolewa upya na kikao cha
konferensi au kamati kuu. Kuwa na kitambulisho au leseni iliyokwisha
muda wake hakumfanyi mtu aliye na vitu hivyo kuwa na madaraka
ya namna yo yote ile.
35
Watumishi
Waliostaafu—Watumishi waliostaafu wanastahili heshima na kufikiriwa kwa
ajili ya kusaidia katika ujenzi wa kanisa la Mungu. Wanaweza kuendelea kubariki
na kusaidia makanisa ambapo kuna ushirika wao kwa njia ya kuchaguliwa
kushika kazi yo yote. Wanaweza pia kufanya kazi za kichungaji
wakiongozwa na kamati ya konferensi.Wachungaji wa Zamani Wasio na
Vyeti—Watu waliowahi kuwekewa mikono kama wachungaji lakini kwa sasa
hawana vitambulisho hai wanaweza kuchaguliwa kuwa wazee wa kanisa na
kama kuwekewa kwao mikono hakujabatilishwa, hawahitaji kuwekewa mikono ya
uzee wa kanisa. Kazi zao zitakuwa zile za mzee wa kanisa mahalia tu.
36
SURA YA 5
Kuunda, Kuunganisha na Kuvunja Makanisa
naMakundi
Kuunda Kanisa
Kanisa huundwa na
mchungaji aliyewekewa mikono kwa pendekezo la kamati kuu ya konferensi.
(Angalia uk. 38 kuhusu utaratibu wa kuunda kundi.) Kwa kuwa kuna mambo
mengi katika uundaji wa kanisa, inapasa mwenyekiti wa Konferensi aalikwe.
Kundi la waumini
waliobatizwa likiwa tayari kubeba majukumu ya kanisa lililoundwa, halina
budi kushauriana na mwenyekiti wa Konferensi na kupata kibali cha kamati
kuu ya konferensi kabla ya kupanga tarehe ya kufanyika kwa uundaji
huo.
Waumini waliobatizwa
wanapokutana siku ile iliyopangwa, itampasa mtu anayeendesha shughuli hiyo
kutoa muhtasari wa imani za msingi za Waadventista wa Sabato.
Kisha yule anayesimamia
shughuli hiyo atatoa wito akiwataka wote wanaokubaliana na kanuni hizo na
ambao wanataka kuungana katika ushirika wa kanisa waje, mbele. Jina la
kila mtu litaandikwa. Kama kuna watu ambao tayari ni washiriki wa kanisa
la konferensi au kanisa lingine, yule anayesimamia shughuli hiyo
atawasilisha barua za uhamisho walizopata. Wale wanaohamia
watakuwa waanzilishi wa kanisa hilo jipya.
Lakini kama hakuna
washiriki wanaohamia, basi washiriki watatu (hasa washika Sabato
waliothibitishwa miongoni mwa watu waliopo) watachaguliwa kuwa
waanzilishi. Wanaweza kuulizwa maswali yafuatayo: Je, mnamkubali Kristo
kuwa Mwokozi wenu? Je, mnakubaliana kikamilifu na kanuni za imani
zilizowasilishwa
hivi karibuni? Je,
mmebatizwa kwa kuzamishwa majini? Je, mna msimamo mzuri na kuaminiana?
37
Kama wakijibu maswali
haya kuwa kukubali, watu hao watatu watatangazwa kuwa waanzilishi wa
kanisa hilo jipya. Kisha majina yaliyokuwa yameandikwa yatasomwa moja
baada ya lingine, kila mtu ataulizwa maswali yaliyoandikwa katika aya
iliyotangulia, na yule msimamizi atapigisha kura miongoni mwa wale waanzilishi,
kumpokea kila mtu katika
ushirika wa kanisa. Kila mtu atakayepokelewa kwa njia hiyo, atakuwa
mshiriki wa kanisa na ana haki ya kulipigia kura jina linalofuata.
Tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa kuhakikisha kuwa ushirika kamili na
upendo wa udugu unakuwepo miongoni mwa wale wanaopokelewa katika ushirika.
Endapo kutatokea tatizo lo lote juu ya suala lo lote, ama la mafundisho,
au ushirika, inapasa hatua ziahirishwe isipokuwa kama suala hilo linaweza
kusuluhishwa kwa upole na busara.
Baada ya waanzilishi
kuwapigia kura washiriki watarajiwa wote, kanisa litakuwa taasisi kamili
likiwa tayari kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi. Washiriki watachagua
kamati ya mapendekezo na mchungaji anayesimamia atakuwa mwenyekiti. Kamati
ya mapendekezo italeta mapendekezo ya kujaza nafasi mbalimbali za uongozi
kanisani. Maofisa hao wakisha kuchaguliwa,
wazee hawana budi kuwekewa mikono kama watakuwa wahajawahi kuwekewa.
Huduma kama hiyo, lakini fupi zaidi itapasa kufanyika kwa ajili ya
kuwawekea mikono mashemasi wa kiume na wa kike.
Hapo kanisa litakuwa
limeundwa kikamilifu na kuwa tayari kwa ajili ya huduma. Kabla ya
mkutano wa uundaji wa kanisa kumalizika, washiriki watapiga kura ya
kuiomba konferensi kulipokea kanisa hilo lililotoka kuundwa katika jumuiya
ya makanisa katika kikao cha konferensi kitakachofuata. Ili
kuhakikisha mafanikio makubwa ya kanisa hilo jipya, inawapasa viongozi wa
konferensi na wa kanisa mahalia kuhakikisha kwamba viongozi wote
wamefundishwa vyema kuhusu kazi zao. Kanisa halina budi pia kuwa na vifaa
vinavyohitajika kwa ajili ya Meza ya Bwana, ambayo, ikiwezekana, ifanyike
kama sehemu ya mkutano huo wa uundaji wa kanisa. Itampasa mhazini,
karani, na viongozi wengine kupokea nyaraka zote muhimu au vifaa vinavyohitajika
kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
38
Kuunda Kundi
Mahali ambapo kuna
waumini kadhaa walio mbali na kanisa, wanaokaa katika eneo moja au walio
katika kundi dogo, wanaoabudia nyumbani au kundi la waongofu wapya,
inawapasa kufikiria kuunda kundi la waumini kwa ajili ya ushirika, ibada
na
utume kwa lengo la kukua
na kuwa kanisa lililoundwa au kuzaa makanisa mengine ya nyumbani katika
eneo hilo la kijiografia. Hadhi ya kuwa kundi huidhinishwa kwa uamuzi wa
kamati ya konferensi, ambayo ikibidi, inaweza kulivunja kundi hilo.
Inapasa divisheni na/au konferensi iwe na mwongozo ulioandikwa kwa
ajili ya kuunda makundi katika eneo lake. Washiriki wa kanisa ambao
ni sehemu ya makundi madogo au makundi ya nyumbani wanaweza kuwa
waanzilishi wa kundi jipya.
Ushirika wa watu
wanaotaka kuwa sehemu ya kundi, utakuwa ama katika kanisa la konferensi au
katika kanisa mahalia (kanisa mama). Kama ushirika wa wale wanaotaka kuwa
sehemu ya kundi itabidi uwe katika kanisa la konferensi, kamati ya
konferensi itapitisha uhamisho wa ushirika wao kwenda kwenye kanisa la
konferensi na kuonesha kuwa wao ni sehemu ya kundi hilo jipya.
Kamati ya konferensi
inapoidhinisha kuanzishwa kwa kundi jipya, timu ya viongozi haina budi
kuteuliwa, ikiwa ni pamoja na mkuu wa kundi, karani, na mhazini. Uteuzi
huo hauna budi kufanywa na mchungaji wa mtaa, au mchungaji mwingine
aliyechaguliwa na kamati ya konferensi, kwa kushauriana na kundi
linaloanzishwa.
Uteuzi mwingine wote
katika kundi hilo utafanywa kwa kura za watu wanaounda kundi hilo.
Mchungaji wa mtaa au mtu mwingine ye yote aliyeidhinishwa na kamati ya
konferensi atakuwa mwenyekiti katika kikao hicho. Washiriki hai wa kanisa
la Waadventista wa Sabato tu ndio wanaweza kuteuliwa.
Mkuu wa kundi hatawekewa
mikono kwa ajili ya kazi hiyo na hatakuwa na mamlaka ya kufanya kazi
ambazo hufanywa na mzee wa kanisa. Hata hivyo, mazingira yasiyo ya kawaida
yakilazimisha kamati ya konferensi inaweza kuteua mtu mwenye uzoefu
kanisani na uwezo wa uongozi kuwa mzee wa kanisa wa kundi hilo. Karani wa
kundi ataweka kumbukumbu ya shughuli na mikutano yote ya kundi na atatuma
taarifa za mara kwa mara za takwimu kwa kanisa mama au kwa katibu mkuu wa
konferensi. Taarifa hizo hazina budi kuwa na takwimu za mahudhurio na shughuli
za kundi, ikiwa ni pamoja na huduma za jamii zinazofanywa katikati ya
juma au siku ya Sabato.
39
Mhazini wa kundi ataweka
kumbukumbu za pesa zote zilizopokelewa na kutumika na atatuma zaka na
sadaka zote ambazo hazikukusanywa kwa ajili ya matumizi mahalia mara moja,
au kwa wakati uliopangwa na konferensi, kwa mhazini wa konferensi ambaye
pia ni mhazini wa kanisa la konferensi. Kama washiriki wa kundi lililoundwa ni
washiriki wa kanisa la konferensi, kundi hilo halitakuwa na haki ya
kufanya marudi au kuhamisha na kupokea washiriki. Masuala hayo yote
yatapelekwa
kwenye kamati ya
konferensi, ambayo ndiyo baraza la kanisa la konferensi. Mwenyekiti wa
konferensi ndiye mzee wa kanisa la konferensi. Kama konferensi itaunda
kundi kwa njia ya kanisa mama la jirani badala ya kanisa la konferensi,
kazi zilizoorodheshwa hapo juu (kama vile kutoa taarifa na ushirika)
zitashughulikiwa na/
kupitia kanisa mama. Kwa
kuwa kundi halina budi kutaka kukua na hatimaye kutambuliwa kama kanisa,
uongozi wake hauna budi kuwaandaa washiriki kwa ajili ya kuwa na hadhi ya
kanisa kwa kuhamasisha shughuli zote zinazofanywa na kanisa.
Kuunganisha Makanisa Inapoonekana
kuwa ni vyema kuunganisha makanisa mawili, kamati ya konferensi haina budi
kupendekeza jambo hilo. Italipasa kila kanisa kuamua kwa kura juu ya suala
la kuungana katika kikao kilichoitishwa rasmi kikiongozwa na mwenyekiti wa
konferensi au mchungaji wa mtaa au mchungaji mwingine aliyewekewa mikono.
Uamuzi wa kukubaliana na jambo hilo ukisha kufanywa na makanisa yote
mawili, itabidi uandaliwe mkutano wa pamoja, ukiongozwa na mwenyekiti wa
konferensi, na kama hayupo, mchungaji aliyewekewa mikono atakayechaguliwa
na konferensi.Tamko lililoandikwa kwa makini litaandaliwa likieleza sababu
za kuungana na mambo mengine muhimu au masharti yatakayokuwapo, kama vile
matumizi, mgawanyo au namna ya kushughulikia rasilimali, na uwajibikaji
juu ya madeni. Linapaswa
40
kutaja jina jipya la
kanisa lililounganishwa na kusitisha kazi za viongozi wa makanisa yote
mawili. Kukubaliwa kwa tamko hilo na mkutano wa pamoja utakuwa mwanzo
wa mwungano wa makanisa hayo mawili. Baada ya hapo itawapasa washiriki wa
kanisa jipya kuchagua kamati ya kupendekeza maofisa watakaohudumu kwa
sehemu ya mwaka huo itakayokuwa imebakia. Nakala ya tamko hilo
itahifadhiwa na konferensi.Washiriki wote wa makanisa hayo mawili wataungana
katika jumuiya hiyo mpya. Hairuhusiwi kuondoa mshiriki ye yote kwa kukosa
kumweka katika orodha ya washiriki wakati wa kuungana. Jumuiya iliyoungana
itawajibika kwa ajili ya utaratibu na marudi ya washiriki wote. Washiriki
walio chini ya marudi watakuwa hawana budi kushughulikiwa kama
ilivyoelezwa mahali pengine katika mwongozo huu. Kumbukumbu zote za
makanisa yote mawili zitakuwa sehemu ya kumbukumbu za kanisa la muungano.
Konferensi mahalia itajulishwa ili ichukue hatua stahiki katika mkutano
mkuu unaofuata.Kuvunja au Kuondoa Makanisa “. . . Kristo naye alivyolipenda
Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa
maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala
kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na waa. ...
Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na
kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya
mwili wake” (Efe. 5:25-30). Moyo huo ndio upasao kutawala katika juhudi za
kusaidia kanisa lililokosa na aina zote za marudi yanayoweza
kufanyika—wakati wote kusaidia na kuokoa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hadhi
ya kuwa kanisa si lazima iwe ya kudumu. Kanisa linaweza kuvunjwa au
kuondolewa katika jumuiya ya makanisa kwa sababu zifuatazo:
Kupoteza Washiriki—Licha
ya juhudi za kulilinda kanisa, wakati mwingine, washiriki wengi hupotea
kwa kuhama au kwa kifo au kwa uasi kiasi kwamba kuwepo kwa kanisa huwa
hatarini. Katika hali kama hiyo, itabidi konferensi ipendekeze
uwezekano wa kuvunjwa kwa kanisa hilo.
41
Kabla kanisa halijafanya
uamuzi wa mwisho wa kuvunjwa, washiriki waliobaki wataombwa kuhamishia
ushirika wao kwenye makanisa mengine. Kama watakuwa wamebaki
washiriki wa kutosha, kanisa linaweza kuitisha mkutano mkuu chini ya
uongozi wa mwenyekiti wa konferensi au mchungaji atakayechaguliwa na
mwenyekiti wa konferensi, kupitisha barua zinazoomba uhamisho wa
washiriki wote hai ili wajiunge na makanisa mengine. Kwa njia hiyo
kanisa litakuwa limejivunja lenyewe kwa mapendekezo ya kamati ya konferensi,
na itakuwa imefunguliwa njia kwa kamati ya konferensi kuchukua hatua ya
kuandika taarifa za kuvunjwa kwa kanisa hilo.
Kama, kulingana na maoni
ya kamati ya konferensi, kuna washiriki wachache mno kufanya mkutano mkuu,
kamati ya konferensi itakuwa na mamlaka ya kupitisha uhamisho wa
washiriki hai kwenda makanisa mengine au kwenye kanisa la
konferensi. Kwa njia hiyo kanisa hilo litakuwa limevunjwa. Kama wakati wa
kuvunjwa kwa kanisa hilo kutakuwa na washiriki walio katika marudi na
hivyo hawawezi kupewa barua zinazosema kuwa wako hai, ushirika wao
utahifadhiwa kwa muda katika kanisa la konferensi wakati uongozi wa konferensi
unahakikisha kuwa kila juhudi imefanyika kuwasaidia washiriki hao haraka
iwezekanavyo kuwa na Ukristo wa kuridhisha. Juhudi hizo zikifanikiwa,
ushirika wao unaweza kuthibitishwa wakati huo katika kanisa la
konferensi au barua za uhamisho zitatolewa ili wahamie katika
makanisa mengine. Kama hawataweza kurejeshwa, itabidi waondolewe katika
ushirika kwa uamuzi wa kamati ya konferensi.
2. Marudi—Matukio ya
kuondoa makanisa kwa sababu za kinidhamu ni machache sana, kwa sababu kazi
ya kanisa ni kutafuta na kuokoa. Kunapokuwa na matatizo makubwa kama vile
uasi, kukataa kuenenda kulingana na Mwongozo wa Kanisa, au uasi dhidi ya
Konferensi ukiendelea, juhudi za dhati hazina budi kufanyika kuepuka haja
ya kuondoa kanisa. Inampasa mchungaji kujitahidi kuimarisha hali ya kiroho
ya kanisa kwa njia ya mahubiri na huduma ya kuwatembelea washiriki.
Konferensi
42
haina budi kuhimiza
mfululizo wa mikutano ya uamsho kuwafanya washiriki wafanye upya agano na
Bwana wao. Kama juhudi hizo hazitafanikiwa, mchungaji, atashauriana na
uongozi wa kanisa, kwa kushirikana na konferensi, akijaribu kuleta suluhu
na upatanisho na kulinusuru kanisa. Hatua hizo za suluhu ni bora
kuliko kuruhusu kudorora kwa uhusiano, jambo ambalo litasababisha
kuondolewa kwa kanisa. Lakini kama juhudi zote za kulinusuru kanisa
zikishindwa, kamati ya konferensi italiangalia kwa makini suala la
kuondolewa kwa kanisa husika. Kama itaamuliwa hatua hiyo ichukuliwe, konferensi
itafuata hatua zifuatazo:
a. Uamuzi wa kupendekeza
kuondolewa kwa kanisa, pamoja na sababu zake, utawasilishwa kwa kanisa
lenyewe katika mkutano mkuu kwa ajili ya
taarifa na kufikiria kwa makini.
b. Kama kanisa
halitakubaliana na pendekezo hilo, linaweza kujibu kwa njia moja kati ya
hizi zifuatazo:
1) Kurekebisha mambo
yaliyosababisha marudi na kukubaliana na maagizo ya konferensi,
kuiomba konferensi itangue pendekezo la kulivunja au kuliondoa kanisa.
2) Kukata rufaa kwenye
kamati tendaji ya union, au divisheni kama ni suala la jumuiya ya
makanisa, ili ifanye usuluhishi kwa niaba ya kanisa hilo.
c. Kama kanisa hilo
litaendelea kuasi, kamati kuu ya konferensi itatoa pendekezo la kuvunjwa
kwa kanisa hilo katika mkutano mkuu wa kawaida wa konferensi au
mkutano mkuu maalum wa konferensi.
d. Kama mkutano mkuu huo
utatoa uamuzi wa kuliondoa kanisa hilo, konferensi itatekeleza
uamuzi huo. Utunzaji wa Washiriki, Nyaraka, na Pesa Washiriki waaminifu wa
kanisa lililovunjwa au kuondolewa wanaweza kutaka kendelea na ushirika
katika Kanisa. Ili kuhakikisha ustawi wao, ushirika wao utahifadhiwa kwa
muda wa hadi mwaka mmoja katika kanisa la konferensi kutoa fursa kwa
43
wale wanaotaka, kuwa na
ushirika katika kanisa la konferensi au kuuhamishia katika kanisa lingine.
Uaminifu wao utatathminiwa na kamati ya konferensi, na ukiridhisha, kamati
ya konferensi inaweza kupendekeza wapewe ushirika katika kanisa la
konferensi au makanisa watakayotaka wenyewe. Majina ya washiriki wa kanisa
lililovunjwa au kuondolewa ambao watakuwa katika marudi yatapelekwa kwa
katibu wa konferensi kwa ajili uangalizi wa kamati ya konferensi
tangu mwanzo kama ilivyoelezwa katika “Kupoteza washiriki,” hapo juu. Kanisa
likivunjwa au kuondolewa kwa sababu ya kupoteza washiriki au sababu za
kinidhamu, sadaka zote, mahesabu ya fedha, na mali zisizohamishika au
zinazohamishika, ziwe katika jina la kanisa mahalia au la konferensi au
jumuiya nyingine halali ya kikanisa, zitakuwa katika dhamana ya
konferensi. Kwa hiyo, konferensi itakuwa na haki, mamlaka na wajibu wa
kusimamia, kulinda au kutumia mali na pesa hizo. Nyaraka zote za kanisa
hilo zitakuwa katika uangalizi wa katibu na/au mhazini wa konferensi. Endapo
hakutakuwa na suala la kinidhamu, njia nyingine badala ya kulivunja au
kuliondoa kanisa ni kulirudisha katika hadhi ya kundi. Uamuzi huo
utafanywa kwa zaidi ya nusu ya kura zitakazopigwa katika kamati ya
konferensi, baada ya kushauriana na mchungaji wa mtaa pamoja na washiriki,
na kuwasilishwa kwa kanisa na mchungaji au mwakilishi wa konferensi. Barua
za uhamisho wa washiriki wote waaminifu zinaweza kupitishwa katika mkutano
mkuu kwenda kwenye kanisa la konferensi au makanisa mengine endapo
washiriki wengine watataka kuhama. Katika mkutano huo huo, mchungaji,
akishauriana na washiriki mahalia, atateua timu ya viongozi miongoni
mwa washiriki wa kundi hilo jipya, ikiwa ni pamoja na mkuu wa kundi,
karani, na mhazini. Kwa
maelezo ya masuala mengine yanayohusu uundaji wa kundi, tazama “Uundaji wa
Kundi” uk. 38
44
SURA YA 6
Ushirika
Wajibu nyeti
unaoambatana na ushirika katika mwili wa Kristo unapasa kueleweka vyema
kwa kila mtu anayetaka ushirika wa Kanisa. Wale tu walioonesha kuwa
wamezaliwa upya na kunufaika na hali ya kiroho ndani ya Bwana Yesu,
watakuwa tayari kupokelewa katika ushirika. Inawapasa wachungaji kuwafundisha wale
wanaotaka kuingia katika ushirika, mafundisho ya msingi pamoja na desturi
zinazohusiana na mafundisho hayo, ili waingie katika Kanisa wakiwa na
msingi imara wa kiroho. Ingawa hakuna umri uliotajwa kwa ajili ya ubatizo,
inapendekezwa kwamba watoto wadogo watakaoonesha nia ya kubatizwa watiwe
moyo na kuingizwa katika mpango wa mafunzo utakaowawezesha kubatizwa.
Mtume Paulo anaandika:
“Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa
katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika
mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya
utukufu
wa Baba, vivyo hivyo na
sisi tuenende katika upya wa uzima.” (Rum. 6:3, 4).
Luka pia anaeleza:
“Petro akawaambia, ‘Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu
Kristo,’ … Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile
wakaongezeka watu wapata elfu tatu. (Mdo. 2:38-41). “Washiriki wa kanisa,
wale aliowaita kutoka gizani waingie katika nuru yake ya ajabu, hawana
budi kuonesha utukufu wake. Kanisa ni hazina ya utajiri wa neema ya
Kristo; na kwa njia ya kanisa, hatimaye litadhihirishwa, hata kwa ‘falme
na mamlaka katika ulimwengu wa roho’ onesho kamili na la mwisho la
upendo wa Mungu.”—AA 9.
Ubatizo
Sharti la Kuingia katika
Ushirika—“Kristo ameufanya ubatizo kuwa ishara ya kuingia katika ufalme
wake wa kiroho. Ameufanya kuwa sharti bayana linalopasa kutimizwa na wote
wanaotaka kutambuliwa kuwa wako chini ya mamlaka ya Baba, Mwana na
Roho Mtakatifu. …
45
“Ubatizo ni tendo nyeti kabisa la kuukataa
ulimwengu. Wale waliobatizwa katika jina la Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu, mwanzoni kabisa mwa maisha yao ya Kikristo hutangaza
hadharani kwamba wameacha kumtumikia Shetani na wamekuwa sehemu ya ukoo
wa kifalme, watoto wa mfalme wa mbinguni. Wamelitii agizo lisemalo:
‘Tokeni kati yao, mkatengwe nao, … msiguse kitu kilicho kichafu,’ nao
hutimiziwa ahadi isemayo ‘Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi
mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.’ 2 Wakorintho
6:17, 18.”—6T 91.
Ubatizo ni njia ya
kusimikwa kanisani. Kimsingi ni ahadi ya kuingia katika Agano la Kristo
linalookoa na hauna budi kuchukuliwa kama ukaribisho nyeti, lakini wa
furaha katika familia ya Mungu. Ushirika katika Kanisa unawezekana
katika makanisa yaliyo katika jumuiya ya makanisa yanayotambuliwa na
konferensi fulani
tu. Aina ya
Ubatizo—Kanisa linaamini ubatizo wa kuzamishwa na huwapokea katika
ushirika wale waliobatizwa kwa njia hiyo tu. (Tazama sura ya 14, “Imani za
Msingi za Waadventista wa Sabato.”) Wale wanaokiri hali yao ya kupotea
kama wenye dhambi, wakatubu dhambi zao na kuongoka kwa dhati baada ya
kufundishwa vyema, wanaweza kukubaliwa kama wataradhia wa ubatizo na
ushirika wa Kanisa.
Mafundisho Kamili na
Kupimwa Hadharani Kabla ya Ubatizo—Inawapasa wataradhia, ama mmoja mmoja
au katika darasa la ubatizo, kufundishwa kutoka katika maandiko, juu ya
imani za msingi na desturi za Kanisa pamoja na wajibu wa washiriki.
Inampasa mchungaji kuliridhisha kanisa, kwa kuwapima hadharani, kwamba
wataradhia wamefundishwa vizuri, wamedhamiria kuchukua hatua hiyo muhimu
na kwa mwenendo na tabia wanaonesha ukubali wa hiari wa mafundisho ya
Kanisa na kanuni za mwenendo ambazo ni udhihirisho wa nje, wa
mafundisho
46
hayo, kwani “kwa matunda
yao mtawatumbua” (Mt. 7:20). Kama haiwezekani kuwapima hadharani, basi
wataradhia watasailiwa na baraza la kanisa, au kamati itakayochaguliwa
na baraza, kama vile baraza la wazee, ambao watatoa taarifa kwa
kanisa kabla ya ubatizo.
“Upimaji wa uanafunzi haufanyiki kwa umakini kama ipasavyo kwa wanaojitoa
kwa ajili ya ubatizo. Ni vyema ikaeleweka kama wanataka kuitwa
Waadventista wa Sabato, au wanasimama upande wa Bwana, ili watoke katika
ulimwengu na kutengwa nao, wasiguse kitu kilicho kichafu. Kabla ya ubatizo
inapasa kuwe na uchunguzi wa kina juu ya hali ya wataradhia. Uchunguzi huu
usifanyike
bila upendo na
uchangamfu, bali ufanyike kwa ukarimu, upole ukiwaelekeza waumini wapya
kwa Mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia. Yafanye matakwa ya
injili yaeleweke kwa wataradhia wa ubatizo.”—6T 95, 96.
Kiapo na Ahadi ya
Ubatizo Kiapo cha Ubatizo—Wataradhia wa ubatizo na wale wanaopokelewa
katika ushirika kwa kukiri imani watathibitisha kukubaliana kwao na imani
za msingi mbele ya kanisa mahalia au chombo kingine kitakachochaguliwa
ipasavyo. (tazama uk. 45) Mchungaji au mzee wa kanisa atawauliza
wataradhia maswali yafuatayo, ambao watajibu ama kwa kutamka, kunyosha
mkono au njia nyingine inayofaa kitamaduni.
Kiapo
1. Je, unaamini
kwamba kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, umoja wa Nafsi
Tatu za milele?
2. Je,
unakikubali kifo cha Yesu Kristo pale Kalvari kama dhabihu ya upatanisho
kwa ajili ya dhambi zako, na unaamini kwamba, kwa neema ya Mungu, kwa
kuiamini damu yake iliyomwagika, umeokolewa kutoka katika dhambi pamoja na
adhabu yake?
47
3. Je, unamkubali
Yesu Kristo kama Bwana wako na Mwokozi wako mahususi ukiamini kwamba,
Mungu amekusamehe dhambi zako na kukupa moyo mpya katika Kristo, na unazikataa
njia za dhambi za ulimwengu?
4. Je, unaikubali
kwa imani haki ya Kristo, ambaye ni Mwombezi wako katika patakatifu pa
mbinguni, na unaikubali ahadi ya kukupatia neema ibadilishayo na
uwezo wa kuishi maisha ya upendo yaliyojengwa katika Kristo nyumbani kwako
na mbele za ulimwengu?
5. Je, unaamini
kwamba Biblia ni Neno la Mungu ililovuviwa, kanuni pekee ya Mkristo kwa
ajili ya imani na mwenendo? Je, unaazimu kuwa na muda wa maombi na
kusoma Biblia mara kwa mara?
6. Je,
unazikubali Amri Kumi kuwa ni andiko la tabia ya Mungu na, ufunuo wa
mapenzi yake? Je, unakusudia kuishika sheria hii kwa uwezo wa Kristo aliye
ndani
yako, ikiwa ni pamoja na
amri ya nne inayoagiza kuiadhimisha siku ya saba ya juma kama Sabato
ya Bwana na kumbukumbu ya Uumbaji?
7. Je, unangoja
kwa hamu kuja upesi kwa Yesu pamoja na tumaini lenye baraka ambapo “huu wa
kufa utakapovaa kutokufa” [1 Kor. 15:54]? Unapojiandaa kukutana na Bwana,
je, utaushuhudia wokovu wake wa upendo kwa kutumia talanta zako katika
juhudi mahususi za kuongoa roho na kuwasaidia wengine kuwa tayari
kwa ajili ya kuonekana kwake katika utukufu?
8. Je,
unalikubali fundisho la Biblia la karama za Roho, na je, unaamini kwamba
karama ya unabii ni moja kati ya alama za kulitambua kanisa la
waliosalia?
9. Je,
unakubaliana na muundo wa kanisa? Na je, unakusudia kumwabudu Mungu na
kulisaidia kanisa kwa njia ya zaka na sadaka zako na kwa juhudi zako binafsi
na ushawishi wako?
10. Je, unaamini kuwa
mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu; na je, utamheshimu Mungu kwa
kuutunza,
48
kuepuka kutumia vitu
vyenye madhara; kuacha kula vyakula vyote najisi; kuacha kutumia,
kutengeneza, au kuuza vileo; kuacha kutumia, kutengeneza, au kuuza
tumbaku katika aina zake zote kwa ajili ya matumizi ya binadamu; na kuacha
matumizi mabaya au biashara haramu ya dawa za kulevya au dawa zingine?
11. Je, unazijua na
kuzielewa kanuni kuu za Biblia kama zinavyofundishwa na Kanisa la
Waadventista wa Sabato? Na je, unakusudia, kuyafanya mapenzi ya Mungu
kwa neema yake, kwa kuishi maisha yanayolingana na kanuni hizo?
12. Je, unalikubali
fundisho la Agano Jipya kuhusu ubatizo wa kuzamishwa majini na unataka
kubatizwa hivyo kama udhihirisho wa hadhara imani yako kwa Kristo na
msamaha wake kwa dhambi zako?
13. Je, unakubali na
kuamini kwamba Kanisa la Waadventista wa Sabato ndilo kanisa la
waliosalia linalotajwa katika unabii wa Biblia na kwamba watu wa kila
taifa, jamaa, na lugha wanakaribishwa na kupokelewa katika ushirika wa
Kanisa hilo? Je, unataka kuwa mshiriki wa kanisa hili mahalia ambalo ni
sehemu ya jumuiya ya Kanisa la ulimwengu?
Kiapo Mbadala
1. Je, unampokea
Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako binafsi, na je, unataka kuishi
ukiwa na uhusiano naye unaookoa?
2. Je,
unayakubali mafundisho ya Biblia kama yanavyo-elezwa katika Tamko la Imani
za Msingi za kanisa la Waadventista wa Sabato, na unaahidi kuishi
kuli-ngana na mafundisho hayo
kwa neema ya Mungu?
3. Je, unataka
kubatizwa kama udhihirisho wa hadhara wa imani yako kwa Yesu Kristo,
kupokelewa katika ushirika wa kanisa la Waadventista wa Sabato, na
kulisaidia kanisa na kazi yake kama wakili mwaminifu kwa ushawishi
wako,zaka na
sadaka, na maisha ya
utumishi?
49
Agano la Ubatizo—Kanisa
limezifasiri imani zake 28 za msingi, pamoja na kiapo cha ubatizo na Cheti
cha Ubatizo na Ahadi, kama agano la ubatizo. Nakala iliyochapwa ya agano
hili pamoja na Cheti cha Ubatizo na Ahadi iliyojazwa ipasavyo, itatolewa
kwa wote wanaopokelewa katika ushirika kwa njia ya ubatizo. Cheti stahiki
kitatolewa kwa wale wanaopokelewa kwa njia ya kukiri imani yao. Cheti
cha Ubatizo pamoja na Ahadi zina nafasi ya kutia sahihi kwa mshiriki mpya
kama njia ya kuzikubali ahadi hizo. Baada ya ubatizo, Cheti cha Ubatizo na
Ahadi vitakabidhiwa kwa wataradhia kama hati ya agano. Ahadi zinasomeka
ifuatavyo:
Ahadi
1. Ninaamini kuna
Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ambao ni umoja wa Nafsi Tatu
za milele.
2. Ninaikubali
mauti ya Yesu Kristo pale Kalvari kama dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya
dhambi zangu, na ninaamini kwamba nimeokolewa kwa neema, kutoka katika
dhambi pamoja na adhabu yake, kwa njia ya imani kwa damu yake
iliyomwagika.
3. Ninampokea Yesu
Kristo Kama Bwana wangu na Mwokozi wangu binafsi, na ninaamini kwamba,
ndani ya Kristo Mungu amenisamehe dhambi zangu na amenipa moyo mpya,
nami ninaziacha njia mbaya za ulimwengu huu.
4. Ninaipokea kwa
imani haki ya Kristo, ambaye ni Mwombezi wangu patakatifu pa mbinguni, na
ninaipokea ahadi yake ya neema inayoweza kubadilisha, pamoja na uwezo wa
kuishi maisha ya upendo yaliyojengwa katika Kristo nyumbani mwangu na
mbele za ulimwengu.
5. Ninaamini
kwamba Biblia ni Neno la Mungu lililovuviwa, yaani kanuni pekee ya imani
na mwenendo wa Kikristo. Ninaahidi kutumia muda mara kwa mara katika
maombi na kusoma Biblia.
6. Ninazikubali
Amri Kumi kuwa ni andiko la tabia ya Mungu, na ni ufunuo wa mapenzi yake.
Ninakusudia, kwa uwezo wa Kristo akaaye ndani yangu, kuishika sheria hii,
pamoja na amri ya nne inayoaagiza kuiadhimisha siku ya saba ya juma
kama Sabato ya Bwana na kumbukumbu ya Uumbaji.
50
7. Ninasubiri kwa
hamu ujio wa Yesu uliokaribia pamoja na tumaini lenye baraka “huu
uharibikao utakapovaa kutokuharibika” [1 Kor. 15:54]. Ninapojiandaa
kukutana na Bwana, nitakuwa ninashuhudia wokovu wake utokanao na upendo
kwa kutumia talanta zangu katika juhudi zangu za kuongoa roho na
kuwasaidia wengine kujiandaa kwa ajili ya kuonekana kwake katika utukufu.
8. Ninalikubali
fundisho la Biblia la karama za Roho, na ninaamini kwamba karama ya unabii
ni moja kati ya vigezo vya kulitambua kanisa la waliosalia.
9. Ninaukubali
muundo wa kanisa. Ninakusudia kumwabudu Mungu na kulisaidia Kanisa kwa
zaka na sadaka zangu na kwa juhudi na ushawishi wangu binafsi.
10. Ninaamini kwamba
mwili wangu ni hekalu la Roho Mtakatifu; na nitamheshimu Mungu
kwa kuutunza, nikiepuka matumizi ya vitu vinavyodhuru, na
kuacha kutumia vyakula vyote vilivyo najisi; kuacha
kutumia, kutengeneza, au kuuza vileo; kuacha kutumia,
kutengeneza au kuuza tumbaku katika aina zake zote; na kuacha
matumizi mabaya au biashara haramu ya dawa za kulevya au dawa
zingine.
11. Ninazijua na
kuzielewa kanuni kuu za Biblia kama zinavyofundishwa na Kanisa la Waadventista
wa Sabato. Ninakusudia kuyatekeleza mapenzi ya Mungu, kwa neema yake, kwa..............................................